October 04, 2014

  • MBUNGE KIGOLA AGEUKWA NA WAPIGA KURA MBELE YA WAZIRI NYALANDU



    MBUNGE KIGOLA AGEUKWA NA WAPIGA KURA MBELE YA WAZIRI NYALANDU
    IMG_1275Kigola akifurahi kabla kibao hakijageuka
    Nasifiwe Ponziano Miwoo mbele ya Waziri Nyalandu alipokuwa akihoji
    uadilifu wa mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola
    IMG_1327Waziri Lazaro Nyalandu akisikiliza maelezo katika mkutano huo.
    ……………………………………………………………………………….
    SAKATA la  vibali vya uvunaji miti katika msitu wa Taifa wa Sao Hill
    Mufindi mkoani Iringa limemuweka pabaya mbunge wa  jimbo la Mufindi
    kusini Mendrad Kigola baada ya wapiga kura  wake kumgeuka mbele ya
    waziri maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  kuwa mbunge huyo ni
    mchochezi katika  sakata  hilo.
    Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Igowole juzi
    Kigola alimkaribisha waziri huyo huku akikosoa mgao wa vibali vya
    kuvuna miti katika msitu wa Taifa wa saohill ambao sehemu yake upo
    katika jimbo hilo, ulivyofanywa kwa vikundi vya wajasiriamali wa
    wilaya ya Mufindi.
    Huku akipigiwa makofi ya mara kwa mara yaliyomfanya ashindwe kusimama
    sehemu moja wakati akiongea, Kigola alisema: "sina pingamizi dhidi ya
    watu na vijiji vilivyopata mgao wa mwaka huu."
    "Shida yangu ni mgao uliotolewa kwa vikundi vya wilaya ya Mufindi
    yenye majimbo mawili. Wakati jimbo langu la Mufindi Kusini vimepata
    vikundi 12 kati ya 48, vingine vyote vilivyobaki vimetoka upande
    mwingine. Mheshimiwa waziri, nakuomba ulione hilo," alisema.
    Kauli ya Kigola ilitafsiriwa na baadhi ya watu waliokuwepo katika
    mkutano huo kwamba ilikuwa ikimpiga vijembe mbunge wa jimbo jirani la
    Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa
    Maliasili na Utalii.
    Taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya
    ya Mufindi zinadai kwamba Mgimwa na Kigola hawapikiki chungu kimoja
    ikiwa ni matokeo ya kinachoelezwa na walio jirani na wabunge hao
    kwamba mmoja wao ana wivu wa kisiasa dhidi ya mwenzake.
    Taarifa hizo zisizo rasmi ambazo hata hivyo hazijawahi kutolewa
    ufafanuzi na Kigola mwenyewe zinadai kwamba amekuwa akimuonea wivu
    Mgimwa baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri.
    Wivu huo ndio umepelekea kuchochea chokochoko ya kuhoji uwiano wa mgao
    wa vibali vikiwemo vibali 48 vilivyotolewa kwa vikundi 48 vya wilaya
    ya Mufindi.
    Hoja ya Kigola dhidi ya mgao wa vibali hivyo ilionekana ina mashiko
    kwa muda wote wa mkutano huo mpaka pale Waziri Nyalandu alipotoa ruksa
    kwa wananchi wa kijiji hicho cha Igowole kuuliza maswali.
    Alikuwa Nasifiwe Ponziano Miwoo aliyechafua hali ya hewamara baada ya
    kupata nafasi ya kuuliza swali alilotoa kwa mtindo aliodai wa kujenga
    hoja ili wananchi wamuelewe.
    Akinukuu vifungu kadhaa vya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano huku
    akioanisha na uadilifu wa mbunge huyo Miwoo alisema:
    "Kuna haja ya kuoanisha hoja za mbunge huyu Kigola na uadilifu wake;
    na kuna haja ya kujua mali zinazomilikiwa na mbunge huyu ili tuone
    kama kunasababu kwa familia yake kupata kibali cha kuvuna miti wakati
    baadhi ya vijiji na vya wilaya ya Mufindi na wajasiriamali wake
    wakikosa," alisema.
    Alisema katika orodha ya wanufaika na vibali vya mwaka huu, jina namba
    388 ni la mtoto wa Kigola anayesoma katika moja ya shule bora zilizoko
    wilayani Mufindi.
    Alisema zipo dalili kwamba Kigola alitumia jina la mwanae huyo kupata
    kibali hicho jambo linalojenga mashaka dhidi ya uadilifu wake.
    "Mheshimiwa Waziri tuna mashaka na huyu mtu na kama kila mwaka anajaza
    fomu inayoonesha mali anazomilikia. Kwanini jina la mwanae litumike,"
    Miwoo alisema huku waliokuwa wakimshangilia Kigola wakigeuza kibao na
    kumshangilia yeye.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.