August 02, 2014

  • Simba yawatambulisha Elias Maguri na Shabani Kisiga



    Simba yawatambulisha Elias Maguri na Shabani Kisiga
    Makamu wa Simba Kaburu akiwatambulisha Kisiga na Maguri leo
    Klabu ya Simba leo imewatambuliasha wake wawili kingo Shabani Kisinga na mshambuliaji Elias Maguri kwa ajili ya kuimarissha kikosi chao kuelekea kwenye msimu mpya wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

    Wachezaji hao wametambulishwa makao makuu ya klabu hiyo na makamu wa Rais wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu ambaye amesema zoezi la usajili kwa klabu yao bado linaendelea.

    Kisiga anajiunga na wekundu hao kwa mara ya pili mara baada ya kumaliza mkataba wake na wakata miwa wa Mtibwa Sugar ambao alikuwa nao kwa miaka miwili na sasa akijiunga na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja.

    Kwa Upande wake Maguri ambaye alikuwa akiichezea Ruvu shooting ya Pwani ameingia kandarasi ya miaka miwili.

    Katika hatua nyingine Kaburu amezungumzia kuelekea kwenye tamasha la siku ya Simba ambayo litakuwa tarehe 9 Agosti 2014 amesema kuwa timu ya Ismailia ya Misri sasa haitakuja kucheza na Simba kufiatia klabu hiyo kuiandikia barua klabu Simba ya kwamba itashindwa kuja kwa tamasha hilo kutokana na kwamba timu hiyo bado inajikusanya kwa maandalizi ya kuanza msimu wa ligi nchini Misri na badala yake Zesco ya Zambia watachukua nafasi hiyo. 


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.