Mzee Bugode akiwa amepumzika nyumbani kwake.
MZEE mmoja anayejulikana kwa jina la Bugode Bulahi mkazi wa Sogesca wilayani Magu Mkoa wa Mwanza, anaomba msaada kutokana na maisha magumu anayoishi. Mzee huyo pamoja na maisha magumu aliyonayo pia anasumbuliwa na ugonjwa wa kibofu cha mkojo na anatakiwa kufanyiwa oparesheni.
"Babu sina hela ya matibabu, kama kuna mtu anaweza kunisaidia tafadhali naomba msaada, naumwa, maisha yenyewe ya tabu" alisema.
Kwa yeyote anayeweza kumsaidia awasiliane nae kwa namba 0768646004.
(Picha/Habari: Na Gabriel Ng'osha/GPL)
0 comments:
Post a Comment