August 01, 2014

  • Ripoti ya utafiti wa matokeo ya vita hii ya Israel dhidi ya Palestina



    Ripoti ya utafiti wa matokeo ya vita hii ya Israel dhidi ya Palestina
    Screen Shot 2014-08-01 at                  8.06.10 AM
    Zikiwa ni zaidi ya wiki tatu zimepita toka kuibuka tena kwa vita ya Israel dhidi ya Palestina, mpaka sasa utafiti unaonyesha ni zaidi ya watu 1450 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi.Wanasema miongoni mwa waliofariki ni pamoja na zaidi ya Wananchi 800 wa Palestina, Wanajeshi 56 wa Israel lakini pia vilevile shule 130 zimebomolewa kwa mabomu.Kingine ambacho ni hasara kubwa ni mabomu ya Israel yaliyobomoa
    nyumba/makazi zaidi ya elfu nne ambapo pia kwa upande mwingine Israel imelaumiwa kwa kusababisha mauaji ya ovyo na makusudi kwa kupoteza maisha kwa wasio na hatia wakiwemo watoto ambao walikua wamejihifadhi na wazazi wao kwenye shule zinazomilikiwa na Umoja wa mataifa ambazo pia zilishambuliwa.

    Wapalestina hawa walilazimika kujihifadhi kwenye shule za umoja wa mataifa baada ya makazi yao kushambuliwa.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.