July 25, 2014

  • TEAM IDDI "TEAM TANZANIA" INAOMBA KURA ZENU

     
     
     
     
    Mr. Iddi Sandaly,
    Bachelors in Accounting, MBA, CPA, CGMA
    Controller at
    Property Management Company
    KUSHIRIKIANA NA KINA MAMA NA WATANZANIA WOTE HAPA DMV

    Kwa miaka mitatu mfululizo nimekuwa nikishiriki na kushirikiana na kikundi cha kina mama kwenye matembezi hiari ya Kansa.
    Kikundi cha kina mama wa DMV ndani yake kukiwa na watanzania wenzetu walio pitia janga la Kansa wamekuwa mbele kuwaomba na kuwataka watanzania wachangie kwenye utafiti wa Kansa na pia kuwaomba watanzania wote wafanyiwe uchunguzi wa Kansa.
    Na kwa miaka mitatu toka kikundi hichi cha wana DMV kilipoanza nimekuwa nikishirikiano nao kwa kutoa mchango wa kifedha kwenye utafiti wa Kansa na pia kwa kuwa nao kina mama wa hawa kwenye matembezi.
    Lengo na Mipango ni kushirikiana na kikundi hiki cha kinamama na kwa mwaka huu nitashirikiana nao na kuandaa na tutajaribu kuwaleta wataaalamu na huduma ya bure ya uchunguzi wa kansa kwa wana DMV kama nilivyoshirikiana na viongozi wenzangu na Nesiwangu kwenye kuleta huduma ya Bure ya Afya hapa DMV.
    Pia tunafanya maandalizi ya mwakani lili tuweze kupata kina baba wengi kujumuika kwenye Matembezi haya ya Kansa,
    DMV KWANZA.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.