kaimu sheikh wa mkoa wa Iringa Abubakar Chalamila |
Waumini wa dini ya kiislamu mjini Iringa wakiwa katika ibada ya idd uwanja wa Samora leo |
Ibada ya idd ikiendelea katika uwanja wa Samora mjini Iringa leo |
Waumini wa dini ya kiislam Manispaa ya Iringa wakiswali pamoja ibada ya Idd leo |
Waumini wa dini ya Kiislam Iringa wakiwa katika ibada |
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza wa tatu kushoto akishiriki ibada ya Idd |
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akiwa na Sheikh Wanguvu kulia mara baada ya ibada ya Idd |
Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Iringa mjini Ibrahim Ngwada akiwa na mmoja kati ya watoto walioshiriki ibada ya Idd wakipongezana kwa kumalizika kwa mwezi mtukufu |
Furaha ya Idd Iringa |
Wazee maarufu na makada wa CCM ambao ni waumini wa dini ya Kiislam wakipiga picha ya pamoja na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza kulia wa pili kulia ni Mr Mbata |
katibu mkuu wa watuma salam mkoa wa Iringa Mood Mambo akifurahia jambo baada ya kumalizika kwa swala ya Idd leo |
Wadau maarufu wa matukiodaioma Iringa katika picha ya pamoja |
Mzee wa matukiodaima wa pili kulia akiwa na wadau wake |
Na MatukiodaimaBlog
WAKATI matukio ya uvurugaji wa amani yanayohusishwa na vitendo vya ugaidi yakiendelea kuota mbawa nchini , kaimu sheikh wa mkoa wa Iringa Abubakar Chalamila amewataka waislamu na viongozi wa dini zote nchini kuendelea kuliombea Taifa huku akidai kuwa matukio hayo ya ugaidi yanayoendelea hayana mahusiano na dini yoyote isipo kuwa wapo baadhi ya wana siasa wanatumia mwanya huo kwa matakwa binafsi ya kuligawa Taifa.
Akizungumza jana mara baada ya swala ya Idd iliyofanyika katika uwanja wa Samoraka Sheikh Chalamila alisema siku zote toka nchi inapata uhuru wake mwaka 1961 dini ya Kiislam na kikristo zilikuwepo na hakukuwa na matukio ya kigaidi kama yanayojitokeza sasa kwa maparoko na masheikh kuvamiwa na kumwangiwa tindikali na hata baadhi ya maeneo kutokea milipuko ya mabomo kama mkoani Arusha na Zanzibar .
Kwani alisema iwapo kungekuwa na vita za kidini kama zilizo nchi inyinge duniani kweli akiwa kama kiongozi wa dini angekuwa ni mtu wa kwanza kuamini kuwa matukio hayo ya kigaidi yanayotokea yanamahusiano ya karibu na dini ila uongozi wa nchi yetu toka hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais wetu Jakaya Kikwete wameendelea kuliunganisha Taifa na kuwa pamoja bila kuwepo kwa misuguano ya kidini .
" Sasa kama watanzania tu wamoja kwa muislamu na Mkristo kukaa pamoja kama ilivyo hivi iweje ugaidi uwepo ......ugaidi kati ya dini na dini hutokea pale penye tofauti na misuguano ila katika Taifa letu hakuna misuguano baina ya waislam na wakristo kila mmoja ana abudu kwa uhuru ....ila wapo watu siwezi kusema moja kwa moja kama ni wana siasa ama vipi ila wapo wanaotaka kutugawa kwa misingi ya dini ili kufanikisha mambo yao ya kisiasa ama ya kiuchumi "
Hivyo alisema ili kuweza kubaini mbaya wetu anayesababisha machafuko nchini ni vema viongozi wa dini zote na serikali kukaa meza moja ili kutafuta mchawi wetu kabla ya kumwacha aendelee kufanya hivyo kwa iwapo ufumbuzi hautapatikana na mtu huyo ama watu hao wakifanikiwa kutugawa basi ni wazi nchi itaingia katika machafuko mabaya zaidi.
" Nafasi bado tunayo nawaomba viongozi wa serikali watuite viongozi wa dini ili tukae kwani watu hawa wanataka kutuvuruga kwa misingi ya kisiasa ama udini .."
Akielezea kuhusu mwenendo wa Taifa alisema kuwa hali si nzuri kutokana na watu kukwepa maadili ya Taifa letu na ndio sababu ya majanga mbali mbali yanaendelea kujitokeza na hivyo kutaka watanzania kurejea katika maadili ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini kuzidi kuhubiri amani na kuliombea Taifa.
Katika hatua nyingine Sheikh Chalamila alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa madai kutoka kwa baadhi ya watu kuwa waislamu si wamoja kutokana na kutofautiana siku ya kuswali Idd ila ukweli ni kuwa waislam ni wamoja na wameshikamana isipo kuwa tofauti ya kuanza kufungua inatokana na matawi katika dini hiyo kama zilizodini nyingine hivyo si jambo la kuwaona kama hawapo pamoja
0 comments:
Post a Comment