July 25, 2014

  • PICHA ZA MH.VICKY KAMATA ALIPOKUTANA NA WAKUU WA SHULE KUJADILI CHANGAMOTO ZA ELIMU GEITA




    PICHA ZA MH.VICKY KAMATA ALIPOKUTANA NA WAKUU WA SHULE KUJADILI CHANGAMOTO ZA ELIMU GEITA
    Picha Habari na Steven Mruma [Geita]
        Walimu mkoani Geita wnakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine zinachangia kurudisha nyuma elimu ya mkoani Geita. Hayo yamezungumzwa na baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano wa kujadili changamoto za elimu mkoani Geita,
          Wakizungumza katika mkutano huo walimu walizitaja changamoto mbalimbali ikiwemo Upungufu wa Nyumba za wafanya kazi, ukosefu wa vyoo kulingana na idadi ya wanafunzi, vyoo vyenye ubora mdogo sana hivyo kuzua hofu ya maambukizi ya magonjwa,  uchakavu wa baadhi ya nyumba za walimu, walimu kucheleweshewa posho na madai yao nk.
           Akizunguza na walimu hao Mh. Vicky kamata aliwasihi walimu kua na moyo wa subira wakati serikali inaweka mikakati ya kutatua matatizo hayo yote huku pia akiwatia moyo wazidi kua na moyo wa kuwafundisha watoto ili Geita iweze kufanya vizuri kwa ngazi ya mkoa na kitaifa.

    Kikao cha pamoja kati ya wakuu wa shule wilayan Geita kujadili changamoto mbalimbali za Elimu.
    Mh. Vicky akizungumza na wakuu wa shule Geita
    Sehemu ya waalimu wakifuatilia kiko kwa makini
    Wakuu wa shule wakifuatilia kikao hicho kwa Makini
    Mh. Vicky akizungumza na wakuu wa shule



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.