
Mwanamke raia wa Sudan   aliyesamehewa adhabu ya kifo baada ya kubadili dini amesafirishwa hadi nchini   Italia baada ya kuwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Khartoum kwa zaidi ya   mwezi mmoja.Meriam Yahia Ibrahim Ishag na familia yake waliondoka na ndege ya   serikali ya Italia wakiongozana na Waziri wa nchini Italia Lapo Pistelli Baba wa   Meriam ni muislamu na kwa Misingi ya sheria ya dini hiyo nchini Sudan Meriam pia   ni muislamu na hawezi kubadili dini.
Aliyebadili dini Sudan   akutana na Papa Francis
  Meriam mwenyewe   alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa   muislamu.Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia, aliweka picha yake na   Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kuwa wanaelekea kutua mjini   Roma.
  Mume wa Meriam Daniel   Wani, ni mkristo,ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa   Marekani.
  Mtoto wa Meriam, Maya   alizaliwa gerezani mwezi May, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua   iliyosababisha ghadhabu dunia nzima.
  Aliachwa huru mwezi Juni   baada ya kuwepo kwa   mashinikizo.
 
.jpg) 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment