July 21, 2014

  • MANCHESTER UNITED YAREJESHA MAJESHI KWA VIDAL …yamwandalia mshahara wa £200,000 kwa wiki


    MANCHESTER UNITED YAREJESHA MAJESHI KWA VIDAL …yamwandalia mshahara wa £200,000 kwa wiki

    Arturo Vidal

    MANCHESTER United imeamua kukomaa na dili la kusaka saini ya kiungo wa Juventus Arturo Vidal na kuahidi kumpa mshahara mnono utakaolingana na wa Robin van Persie.

    United sasa ipo tayari kuweka mezani pauni milioni 40 kwaajili ya Vidal pamoja kumlipa mshahara wa pauni laki 2 kwa wiki.

    Mshahara huo utamuweka meza moja na Robin van Persie ambapo kimshahara watazidiwa na Wayne Rooney pekee.

    Mkurugenzi wa Juventus Pavel Nedved ameweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuuza Vidal lakini hawatakuwa na namna ya kukataa kumpiga bei iwapo United itakuja na ofa nono.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.