July 27, 2014

  • Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (pichani) amesema kuwa mchakato wa Mabadiliko ya Katiba umefikia ulipo sasa, kutokana na makosa matatu makubwa yaliyofanywa na vyama vya siasa.


    Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (pichani) amesema kuwa mchakato wa Mabadiliko ya Katiba umefikia ulipo sasa, kutokana na makosa matatu makubwa yaliyofanywa na vyama vya siasa.
     Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku
    ---
     Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (pichani) amesema kuwa mchakato wa Mabadiliko ya Katiba umefikia ulipo sasa, kutokana na makosa matatu makubwa yaliyofanywa na vyama vya siasa.

    Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo aliwataka viongozi wakuu wa Serikali na wale wa vyama vya siasa nchini, wasikubali kushindwa kukamilisha mchakato huo.
    Akizungumza kwenye Mahojiano Maalumu na gazeti hili yaliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Butiku aliyekuwa pia Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema kuwa bado hakuna sababu ya msingi ya kushindwa kukamilisha mchakato huo.
    "Pamoja na yote yaliyotokea, sisi kama taifa, hasa viongozi wakuu wa taifa katika Serikali na vyama, tusishindwe kuandaa Katiba Mpya. Hatuna sababu ya msingi ya kushindwa," alisema Butiku.
    Kauli hiyo ya Butiku imekuja huku zikiwa zimesalia takriban siku 10 kabla ya Mkutano wa Pili wa Bunge Maalumu la Katiba, unaotarajiwa kuanza Agosti 5 mjini Dodoma.
    Makosa matatu

    Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alisema kuwa kuna makosa matatu ya msingi yaliyofanyika katika mchakato huo wa Katiba Mpya ulio kwenye hatua ya Bunge Maalumu la Katiba.
    Aliyataja makosa hayo akisema:

     "Kosa la msingi na ambalo halisameheki ni kule kuacha mwongozo wa sheria, watu na makundi wakashughulika tu walivyoona wao nje ya mfumo wa sheria. Hilo ndilo kosa kubwa, linaambatana na mengi; Nyerere alisema ukitenda dhambi ya msingi kama kula nyama ya mtu unaendelea nayo."

    Alilifafanua: "Lingine ni kuanza utaratibu wa kubadili taratibu na kanuni zinazotakiwa zizingatie sheria. Mkishafanya hivyo, maana yake kuna mtu anafanya anavyotaka.
     
     Butiku aliongeza: "Ni muhimu sheria ingezingatiwa na hakuna haja kwa vyama vya siasa kwenda katika Bunge la Katiba na rasimu zao kwapani, zikiwa zimefichwa;…huwezi kuwa na maoni nje ya rasimu, yasiyozingatia rasimu iliyowasilishwa."Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.....



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.