Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya soka ya vijana wa TFF Ayoub Nyenzi kwa ajili ya mashindano ya Airtel Rising Stars yanayotariwa kuanza kutimua vumbi ngazi ya mkoa Jumapili ijyayo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana jijini Dar-es-Salaam.
·
Saidi Meck Sadiki mgeni ramsi ufunguzi Jumapili.
Airtel Tanzania Jana Alhamis Julai 24, 2014 imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 18 za wavulana zinazoshiriki michuano ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa jijini Dar es Salaam Jumapili 27 Julai 2014.
Dar es Salaam inajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Washiriki wengine wa mashindano hayo ya kubaini na kuendeleza vipaji watatoka katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Morogoro. Akizingumza katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa iliyofanyika kwenye uwanja cha Kumbu Kumbu ya Karume, Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi amesema maandalizi yamekamilika.
"Tunatajia kuwa na mashindano yenye ushindani mkali na ya kusisimua. Napenda kuchukua fursa hii kuwataka viongozi wa soka ngazi ya mkoa kuhakikisha wanakuwa makini ili kuchagua vijana wenye vipaji kuunda timu zao za mikoa zitakkazoshiriki fainali za taifa zitakazofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao", alisema Nyenzi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars katika mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni utakofanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Jumapili ijayo.
Mkoa wa Mwanza utafungua rasmi michuano yake Agosti 3, ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya ambao umepangiwa kuanza mashindano yake Agosti 4 wakati mkoa wa Morogoro utaanza mechi zake Agosti 5. Wakuu wa mikoa husika wanatarajiwa kuwa wageni rasmi kwenye hafla za ufunguzi wa michuano hiyo.
Mbali na timu za wavulana, mashindano hayo pia yatashirikisha timu za wasichana katika ngazi ya taifa na kufanya fainali hizo kuwa na jumla ya timu 12, sita za wasichana na sita za wavulana. Timu za wasichana zinatoka mikoa ya Ilala, Kinodoni, Temeke, Mbeya, Mwanza na Zanzibar. Huu ni mwaka wa tatu tangu mashindano ya Airtel Rising Stars yalipoanza kushirikisha timu za wasichana.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde amesisitiza nia thabiti ya kampuni ya Airtel ya kuendelea kudhamini programu hii ya vijana na kulipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, wizara inayosimamia michezo na wadau wengine wa soka kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel kusaidia maendeleo ya soka la vijana.
Michuano wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.
Airtel Rising Stars itahitimishwa kwa mashindano ya kimataifa ambayo yatashirikisha wachezaji nyota kutoka nchi 22 barani Afrika ambapo kampuni ya mawasiliano ya Airtel inafanya biashara. Mashindano hayo ya kimataifa yamepangwa kufanyika nchini Gabon kuanzia Agosti 25 hadi 30.
0 comments:
Post a Comment