July 21, 2014

  • PAUNI MILIONI 24 ZA ARSENAL KWAAJILI YA KIUNGO WILLIAM CARVALHO ZAPIGWA CHINI NA SPORTING LISBON




    PAUNI MILIONI 24 ZA ARSENAL KWAAJILI YA KIUNGO WILLIAM CARVALHO ZAPIGWA CHINI NA SPORTING LISBON

    Arsenal, Sporting Lisbon, William Carvalho, AFC,                    BPL, EPL, Premier League, JUHUDI za Arsenal kujiimarisha zimegonga mwamba baada ya ofa yao ya pauni milioni 24 kwaajili ya kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho kupigwa chini.

    Arsenal imedhamiria kuimarisha safu yake ya kiungo lakini inaelekea kukwama baada ya kushindwa kumsajili Sami Khedira wa Real Madrid huku pia ikikumbana na kizuizi kwa William Carvalho.

    Carvalho ana kipengele kinachomruhusu kuondoka kwa pauni milioni 37, lakini Arsenal wanaonekana  hawako tayari kufikia kiwango hicho.

    Manchester United pia walikuwa wanamtaka kiungo huyo lakini wakajiweka kando baada ya kubaini kuwa Sporting Lisbon haikuwa na dalili ya kupunguza kipengele hicho cha manunuzi licha ya kwamba tayari klabu hiyo ya Ureno imeshamsajili Shehu Abdullahi  kama mbadala wa Carvalho.

    Arsenal sasa ni juu yao, kuamua kufikia pauni milioni 37 zinazohitajika au kuangalia njia mbadala.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.