July 27, 2014

  • Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO:Wakati Bunge Maalumu la Katiba linakusudia kufanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wajumbe wa Bunge hilo ambao wamesusia kushiriki mchakato wa Katiba, wanasheria, wasomi na wanaharakati wamepinga dhamira hiyo wakisema itasababisha kuvunjwa kwa Katiba.




    Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO:Wakati Bunge Maalumu la Katiba linakusudia kufanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wajumbe wa Bunge hilo ambao wamesusia kushiriki mchakato wa Katiba, wanasheria, wasomi na wanaharakati wamepinga dhamira hiyo wakisema itasababisha kuvunjwa kwa Katiba.
     Mtaalamu wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Peter Maina
    --
    Wakati Bunge Maalumu la Katiba linakusudia kufanyia marekebisho kanuni zake ili kuwabana wajumbe wa Bunge hilo ambao wamesusia kushiriki mchakato wa Katiba, wanasheria, wasomi na wanaharakati wamepinga dhamira hiyo wakisema itasababisha kuvunjwa kwa Katiba. 

    Wajumbe wanaolengwa katika marekebisho hayo ni wale wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutoka Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na baadhi ya wajumbe kutoka Kundi la 201 walioteuliwa na Rais.
    Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki alisema mabadiliko yanayokusudiwa kufanywa yatahusisha masuala ya nidhamu, yakiwamo fujo na utoro, mambo ambayo hivi sasa hayawezi kudhibitiwa moja kwa moja na mwenyekiti wa Bunge hilo.
    Sitta alikuwa akitoa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake juzi na kusomwa mbele ya waandishi wa habari na Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad, ikieleza maazimio ya kikao cha usuluhishi alichokuwa amekiitisha kwa ajili ya kutanzua mzozo unaotishia kukwamisha mchakato wa Katiba Mpya.
    Taarifa hiyo ilisema kitendo cha Ukawa kuendelea kususia Bunge, kinapuuza wito wa jamii kupitia makundi mbalimbali pamoja na madhehebu ya dini na juhudi za usuluhishi za kutaka kuwezesha vikao vya Bunge hilo viendelee.

    Ukawa walitoka bungeni siku chache kabla ya kuahirishwa kwa awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu Aprili 16 mwaka huu, kwa madai kwamba CCM kinatumia wingi wa wajumbe wake kutaka kufutwa kwa baadhi ya mapendekezo ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.
    Tayari Mwenyekiti Ukawa, Freeman Mbowe na Mwenyekiti Mwenza, Profesa Ibrahim Lipumba wamesisitiza kuwa hawatarejea bungeni hata kama Bunge litafanyia marekebisho kanuni ili ziwabane Ukawa.
    Profesa Maina
    Mtaalamu wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Peter Maina alisema kama wanataka kufanyia mabadiliko kanuni, kinachotakiwa kufanyika kwanza ni kubadili sheria ya mabadiliko ya Katiba ili kanuni zilizokusudiwa kufanyiwa marekebisho zisiwe juu ya sheria.
    "Kanuni za Katiba ni kanuni ambazo zimepitishwa baada ya kupatikana kwa sheria, hivyo wanatakiwa kwanza ama kurejea katika Bunge la Jamhuri kufanya marekebisho ya sheria, kisha ndiyo wafanye hayo marekebisho wanayoyataka ya kanuni," alisema Profesa Maina.
    Aliongeza: "Kinachotakiwa hapa ni watu kuheshimu sheria kama tunataka mchakato huu umalizike salama na tupate katiba bora na yenye kuweka mbele masilahi ya taifa."Kwa habari zaidi Bofya na Endelea........



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.