July 27, 2014

  • KUFUATIA MUAMKO HAFIFU WA UCHANGIAJI DAMU MKOANI RUKWA KUTOKANA NA DHANA POTOFU ZILIZOPO, MADAKTARI WAONYESHA MFANO KWA KUCHANGIA DAMU KATIKA HOSPITALI KUU YA MKOA HUO



    KUFUATIA MUAMKO HAFIFU WA UCHANGIAJI DAMU MKOANI RUKWA KUTOKANA NA DHANA POTOFU ZILIZOPO, MADAKTARI WAONYESHA MFANO KWA KUCHANGIA DAMU KATIKA HOSPITALI KUU YA MKOA HUO
    Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia damu katika zoezi lilioendeshwa na Shrika la Red Cross katika kuchangia damu Mkoani Rukwa. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine uhaba ambao unafikia nusu kwa nusu ukilinganisha kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo. Uhaba huo umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
    Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wkichangia damu.
    Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
    Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
    Dkt. Marwa akichangia damu.
    Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
    Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.
    (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.