Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani.
Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa.
Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema "Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari".
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa. Maombi hayo yalifanyika katika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment