December 12, 2015

  • WATAKAOPANDISHA NAULI KUTUPWA JELA



    WATAKAOPANDISHA NAULI KUTUPWA JELA

    Wananchi wakiwa katika            pilika pilika za usafiri Ubungo.
    WAMILIKI na mawakala wa usafiri wa mabasi yaendayo mikoani wameonywa kutopandisha nauli katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwamo kufungwa jela.

    Onyo hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mohammed Mpinga wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa abiria wa bodaboda kwa njia ya simu ya 'Fasta Fasta Service' ambayo itamwezesha abiria kupata huduma hiyo kwa kufuatwa mahali alipo.
    Kamanda Mpinga alisema imekuwa ni tabia ya wamiliki wa usafiri wa mabasi hayo pamoja na mawakala wao kuongeza nauli hizo kinyume cha sheria na taratibu zilizowekwa jambo ambalo linawaumiza wananchi.
    "Ili kuwabaini watu hawa wanaokiuka sheria hiyo, tumeweka askari kanzu vituo vyote vya mabasi yaendayo mikoani kwa lengo la kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua kali za sheria," alisema.
    Alisema Polisi Kikosi cha Barabarani kimejipanga nchi nzima ili kuhakikisha wanakomesha vitendo hivyo na si tu kwa Kituo cha Ubungo pia kwa kupandikiza abiria watakaokuwa na kazi ya kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika.
    Alisema katika kipindi cha mwaka jana, wamiliki na mawakala watano walifungwa jela kwa kosa kama hilo na kuweka wazi kuwa mwaka huu wamedhamiria kuona kila mmiliki wa mabasi na mawakala wao wa ukatishaji tiketi wanashughulikia suala hilo.
    Akizungumzia kuhusu huduma ya usafiri wa bodaboda ya Fasta Fasta, Kamanda Mpinga alisema huduma hiyo inawarahisishia madereva wa bodaboda kuongeza kipato, kuondoa uhalifu na usalama wa mali zao.
    Aidha, alisema huduma hiyo itamwezesha dereva na abiria kujuana na hata tatizo linapotokea, ni rahisi kujua nani wa kumkamata kwa ajili ya masuala mengine ya kisheria. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Fasta Fasta, Prasad Acharya alisema kwa kuanzia wamezindua huduma hiyo Dar es Salaam na kwamba baada ya Februari mwakani, watazindua 

    HABARI LEO.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.