December 23, 2015

  • MFUMO WA KIELETRONIKI KURATIBU SHUGHULI ZA SERIKALI - MH. MHAGAMA



    MFUMO WA KIELETRONIKI KURATIBU SHUGHULI ZA SERIKALI - MH. MHAGAMA
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akisisitiza umuhimu wa kutafuta majibu ya maswali kwa wakati yaliyoelekezwa Serikalini kipindi cha Bunge wakati alipokutana na Maafisa wa Bunge wa Wizara za Tanzania Bara leo, Tarehe 23 Desemba, 2015, Jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya maafisa Bunge kutoka Wizara za Tanzania Bara wakiendelea na uchambuzi wa maswali yaliyoelekezwa serikalini kipindi cha Bunge leo, Tarehe 23 Desemba, 2015, Jijini Dar es Salaam.
    Mkurugenzi Idara ya Bunge na Siasa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Yona Mwakilembe, akieleza jinsi maafisa Bunge wa Wizara za Tanzania Bara walivyojipanga kutoa majibu kwa wakati maswali yaliyoelekezwa serikalini kipindi cha Bunge leo, Tarehe 22 Desemba, 2015, Jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya maafisa Bunge kutoka Wizara za Tanzania Bara wakiendelea kufuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), alipokutana nao wakati wa uchambuzi wa maswali yaliyoelekezwa serikalini kipindi cha Bunge leo, Tarehe 23 Desemba, 2015, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.