December 05, 2015

  • 'IMETIKI' MAKAMPUNI MANNE YALIYOKWEPA KODI YALIPA ZAIDI YA BILIONI 5


    'IMETIKI' MAKAMPUNI MANNE YALIYOKWEPA KODI YALIPA ZAIDI YA BILIONI 5

    ZIKIWA zimepita siku kadhaa toka Rais Dr John Pombe Magufuli kutangaza kuwa ametoa siku saba kwa makampuni na wafanyabiashara waliokuwa wanadaiwa kodi kuwa wawe wameshalipa kodi zote vinginevyo sheria ingechukua mondo wake,hadi kufikia leo jumla ya makampuni 4 yaliyokuwa yamekwepa kodi wamelipa madeni yao.

    Taarifa kutoka TRA zinasema kuwa makampuni hayo yamelipa jumla ya bilioni 5.23 huku ikisemekana kuwa huenda pesa hizo zikaongezeka zaidi kuanzia leo kwani zimebaki siku 4 tu ili kufika siku saba alizota Magufuli.

    Magufuli juzi wakati akizungumza na wawakilishi wa sekta binafsi na wafanya baishara alisema kuwa pamoja na kwamba Serikali yake itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji wa ndani na wafanyabiashara wa ndani,hatakuwa na simile katika kuwadai kodi kwani bila kufanya hivyo atashindwa kuendesha Serikali


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.