December 04, 2015

  • MAHAKAMA YA MAUAJI YA KIMBARI YAFUNGWA


    MAHAKAMA YA MAUAJI YA KIMBARI YAFUNGWA

    Image copyrightReuters
    Image captionWatutsi 800,00 na Wahutu wenye msimamo wastani waliuawa katika kipindi cha siku 100 tu.

    Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikishughulikia kesi za mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita imefungwa.


    Mahakama hiyo iliyokuwa mjini Arusha Kaskazini mwa Tanzania ilikuwa ikisikiliza kesi za watuhumiwa wakuu wa mauaji hayo ya kimbari.
    Sherehe za siku tatu zimefanyika kuadhimisha kufungwa kwa mahakama hii.
    Waajiriwa wa sasa na wa zamani, mahakimu na mashahidi walikusanyika pamoja kuhudhuria sherehe hizo mjini Arusha
    Baadhi ya matukio katika sherehe hizo yalikuwa ni pamoja na uzinduzi wa eneo la kubarizi al maarufu kama uwanja wa Amani, na kumbukumbu ya wahanga wa mauwaji ya kimbari



    Image copyrightReuters
    Image captionSherehe hizo zitadumu kwa siku tatu.

    Maofisa waandamizi mbalimbali wa serikali ya Rwanda na Tanzania pia walihudhuria sherehe hizo, ikiwa ni pamoja na mshauri maalum wa kuzuia mauwaji ya kimbari wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Adama Dieng.
    Katika uwepo wake wa miongo miwili, mahakama hiyo imetumia takribani dola bilioni mbili, huku ikishughulikia kesi zipatazo 93.
    Hata hivyo, haikuwa safari rahisi ya kutoa haki kwa mahakama hii.
    Mara nyingi iligonga mwamba kupata mashahidi waliokuwa tayari kushuhudia.



    Image copyrightAFP
    Image captionKumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda

    Na hata kama mafanikio yake yamepongezwa na wengi, ambao wamedai pasipo mahakama hiyo ingekuwa vigumu kuwasaka na kuwashtaki watuhumiwa wakubwa wa mauwaji hayo, wakosoaji wa mahakama hii, ikiwa ni pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame, wamedai kwamba mahakama hiyo imefanya kidogo ikilinganishwa na fedha na muda iliyopatiwa
    Bado kuna kesi moja inayohusisha watuhumiwa sita inaendelea na inatarajiwa kutolewa hukumu yake hapo wiki ijayo.
    Lakini hatma ya watuhumiwa wanane ambao waliachiwa huru miaka kadhaa iliyopita bado haijajulikana hadi leo baada ya kukosa nchi wanayoweza kuhamia
    Watutsi 800,00 na Wahutu wenye msimamo wastani waliuawa katika kipindi cha siku 100 tu.
    BBC.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.