December 30, 2015

  • BREAKING NEWZZ: SERIKALI YA MAGUFULI KIBOKO, KIGOGO MWINGINE ASIMAMISHWA KAZI LEO


    BREAKING NEWZZ: SERIKALI YA MAGUFULI KIBOKO, KIGOGO MWINGINE ASIMAMISHWA KAZI LEO


    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    OFISI YA RAIS








    Anuani ya Simu "TAMISEMI" DODOMA
    Simu Na: (026) 2322848, 2321607,
    2322853, 2322420,
    Nukushi: (026) 2322116, 2322146.
    2321013,
    Barua pepe:ps@poralg.go.tz

    Tawala za Mikoa
    na Serikali za Mitaa,
    S. L. P. 1923, DODOMA.
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu fisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.
    Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.
    Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
    Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.
    Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.
    Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.


    Imetolewa na:
    Rebecca Kwandu
    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
    Ofisi ya Rais - TAMISEMI


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.