December 01, 2015

  • Lady JayDee Ndani ya London


    Lady JayDee Ndani ya London
    Na Freddy Macha, London 
    Mwanamuziki na mwimbaji mashuhuri wa Tanzania, Lady JayDee, anatazamiwa kutua jijini London kesho kutwa Alhamisi tayari kwa onesho kabambe Jumamosi. Akizungumza nami Jumatatu usiku, promota wa shoo hilo, Frank Leo, alisema anawaomba Watanzania na marafiki zao wajiunge kumshangilia Mtanzania mwenzetu tarehe 5 Desemba. Kiingilio cha paundi 20 ( wastani wa shilingi 45,000) kitatozwa katika holi maridadi la Oasis Banqueting Suite mtaa wa Barking, Mashariki ya London. Bango la shoo ya 5 Desemba                    2015
    Frank Leo : "Shoo yake ina dhamira ya kuwaweka wana Afrika Mashariki pamoja kusheherekea na kufurahia siku ya Jamhuri, ughaibuni. Tunaiita shoo hii "Wafalme na Malkia" (Kings and Queens) maana ninaamini sisi sote ni wafalme na malkia. Lazima tukumbushane kuwa tunao uwezo kuzidi tunavyojua."
      Mkurugenzi wa Upendo                    Events- Frank Leo 
    Frank Leo na bango la shughuli kadhaa za Upendo Events. Lady JayDee anatazamiwa kukaa Uingereza hadi Jumatatu tarehe 7 atakaporejea nyumbani. Mzawa wa Matombo, Morogoro, Frank Leo Mbena, anayo diploma na shahada ya usafiri na utalii kutoka hapa Uingereza alikosomea na anakoendelea kuishi. Alianzisha shirika la "Upendo Events" karibuni kujenga na kutukuza sanaa na mambo mbalimbali ya Watanzania na Waafrika Mashariki. Onesho la tarehe 5 Desemba litamhusisha pia mbunifu mavazi "All Things Africa" atakayeendesha wasanifu mavazi. Frank Leo na mwenzake 
    Mfano wa mavazi yenye hulka ya Kiafrika ihsani ya "All Things African" Mkurugenzi wa "All Things African", Hamida Mbaga anachangamkia sana jitihada za "Upendo Events" na Frank leo kuitukuza na kuijenga taswira ya Tanzania nje na ndani. F Macha na Hamida Mbaga of                    All Things African- pic by Fab Moses
    Fahari ya Utanzania. Mdau wa Kitoto Blog na Meneja wa "All Things African"- Hamida Mbaga. Picha na Fab Moses Habari zaidi tembelea www.upendoevents.com


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.