August 22, 2014

  • Umeme wa uhakika ndiyo nguzo ya maendeleo ya uchumi nchini – IPTL




    Umeme wa uhakika ndiyo nguzo ya maendeleo ya uchumi nchini – IPTL
     Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), iliyo chini ya Pan Africa Power Solutions (PAP), Bw. Harbinder Sethi (Kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) maboresho yaaliyofanyika katika kiwanda hicho tangu PAP ilipochukua uongozi wa IPTL. Wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya IPTL. 
     Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), iliyo chini ya Pan Africa Power Solutions (PAP), Bw. Harbinder Sethi (Kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) maboresho yaaliyofanyika katika kiwanda hicho tangu PAP ilipochukua uongozi wa IPTL. 
    Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), iliyo chini ya Pan Africa Power Solutions (PAP), Bw. Harbinder Sethi (Kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) maboresho yaaliyofanyika katika kiwanda hicho tangu PAP ilipochukua uongozi wa IPTL.  Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa kampuni hiyo Bw. Parthiban Chandrasakaran.

    Mahitaji makubwa ya umeme nchini yataweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuhakikisha kuna uzalishaji ziada wa umeme kwa kutumia teknolojia zinazokubalika na nishati iliyopo Tanzania.

    Hayo yalisemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), kampuni iliyo chini ya Pan African Power Solutions (PAP) wakati wa ziara ya wandishi wa habari walipotembelea mitambo ya ufuaji umeme ya kampuni hiyo iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 

    Alisema kuwa IPTL inaamini kwamba usambazaji wa umeme unaweza kuboreshwa kutoka megawati 800, ambazo kwa sasa zinahudumia watu zaidi ya milioni 51.1 ambao mahitaji yao yanaweza kuzidi megawati 2000.  

    "PAP/IPTL inaamini kuwa soko bado ni kubwa na si tu IPTL, bali pia na makampuni mengine yanapaswa yachangie katika kukuza uwezo wa gridi na uzalishaji wake ili kufikia matakwa ya watanzania wapatao watu milioni 51.1 kama ilivyokadiriwa katika sensa iliyofanyika mwaka 2014," alisema Bw. Sethi. 

    Alibainisha kuwa kupitia usambazaji wa umeme wa uhakika na sera nzuri ya uwekezaji, Tanzania itapiga hatua ya kimaendeleo kwa kasi na kuwa moja kati ya nchi kubwa kiuchumi Afrika katika siku za karibuni.  

    "Kama wawekezaji watahakikishiwa umeme wenye gharama nafuu na sera nzuri ya uwekezaji inayolinda pande zote mbili, viwanda vingi vitajengwa nchini kwasababu Tanzania imebarikiwa kuwa na wingi wa mali ghafi. Viwanda na miundombinu mizuri ni moja kati ya vigezo ambavyo wachumi utumia katika kutambua maendeleo ya nchi," alisema.  

    Alisema kuwa kuna ushaidi tosha unaoonyesha jitihada za kuhakikisha kuwa nchi inaondokana na umaskini, baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi za kiafrika ambazo uongezekaji wa watu wake umebaki thabiti na kukuwa kwa kasi kwa maendeleo ya watu walio na uchumi wa kati.  

    Ongezeko la uwekezaji katika miundombinu unaongeza mahitaji ya umeme na usambazaji ambao pia unasaidia kukuza viwango vya pato la taifa (GDP).

    Bosi huyo wa IPTL/PAP alisema kuwa kampuni yake ameeleza jitihada zake katika kuongeza uwezo wa umeme nchini kwa kuweka mipango kazi ya utanuzi madhubuti na kupunguza viwango vya tozo katika bei ya umeme kwa kuwajali wateja.  

    "Awamu ya kwanza ya mpango wetu umelenga kuweka mtambo wa megawati 200 wa gesi ambao utakua karibu na mtambo wa sasa wa megawati 103 wa IPTL unaotumia mafuta mazito (HFO). Mazungumzo juu ya hili bado yanaendelea na mamlaka husika. Kama yote yatakwenda vizuri, mpango huu utamalizika ifikapo mwezi Aprili 2015. 

    "Ikiwa kama ni sehemu ya awamu ya kwanza, tutaweka kituo kidogo kipya chenye 220kv ambao ni muhimu sana kwa Tanesco kwa ajili ya usambazaji katika kanda zote mpya mbali mbali za maendeleo huko Bagamoyo na Chalinze. Hii ni pamoja na laini ya 220kv ya Ubungo," alisema. 

    Bw. Sethi alibainisha kuwa awamu ya pili – itakuwa ni uwekaji wa mtambo wa megawati 300 wa gesi pembezoni mwa mtambo wa IPTL.
    Alisema kuwa mtambo wa sasa wa IPTL utaendelea kuendeshwa kwa kutumia mafuta mazito (HFO) endapo kutakuwa na tatizo katika gridi ya taifa hususani la gesi asilia au matumizi ya mafuta. 


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.