July 06, 2014

  • MJUMBE WA KAMATI KUU CCM TAIFA JERRY SILAA ALIPOONGOZA KUSIMIKWA KWA KAMANDA MPYA WA UVCCM MKOA WA MBEYA




    MJUMBE WA KAMATI KUU CCM TAIFA JERRY SILAA ALIPOONGOZA KUSIMIKWA KWA KAMANDA MPYA WA UVCCM MKOA WA MBEYA LIVE!!

    Jioni hii majira ya saa kumi na mbili jioni ndio mkutano wa hadhara umeishia hapa Mbeya mjini ambapo kulikuwa na matukio makubwa ya vijana wa CCM kutoha sehemu mbali mbali za nchi kumunga mkono mwenyekiti mwenzao wa Mbeya ndugu Kajuna katika tukio la kufungua mashina,kusimika makamnda na mkutano wa hadhara

    vijana hao ambao walikuwa wameambatana na mjumbe wa NEC toka Mafya na mkt wa UVCCM mkoa wa Pwani ndugu Muhamedi Nyundo,MNEC wa vijana kupitia Zanzibar Bi Nadra,katibu wa idara ya utawala,uchumi na fedha UVCCM makao makuu na mkt wa UVCCM wilaya ya mjini Zanznibar,COM Paul Makonda ambae ni mjumbe wa bunge la katiba na katibu wa hamasa chipukizi makao makuu
    pia msafara huo ulikuwa pia na mkt wa UVCCM mkoa wa mjini unguja ndugu Kibwana,mkt wa UVCCM mkoa wa Morogoro Bi Harieti Sutta,mkt wa UVCCM mkoa wa Dodoma ndugu Masunga,mkt wa UVCCM mkoa wa Katavi ndugu Calvin Mbogo (mnyama) mkt wa UVCCM wilaya ya Rufiji ndugu Mtweve,mkt wa UVCCM mkoa wa DSM ndugu Omar Matulanga,mjumbe wa baraza kuu UVCCM Taifa kupitia mkoa wa Morogoro ndugu Asenga Abubakar,Mjumbe kupitia mkoa wa Tanga Bi Husna Mbwambo na makada wengine ambao wameonyesha umoja wa hali ya juu katika kukijenga chama chao na kuwa vijana wa mfano KWA VIJANA WENGINE
    pamoja na yote, waliwahasa vijana wa Mbeya kutokurudia makosa,,,kwa walioyapata yana watosha,,,akiongea kada mtiifu wa CCM Bi Juliana Shonza alizitaja ahadi zote za mbunge Sugu ambazo hadi sasa hajatekeleza hata moja,,,mfano mabwawa ya samaki kwa vijana,,,,
    KADA Mtelea Mwampamba aliongea historia ya CCM na CHADEMA,,,na kuwa hasa Wanambeya daima wasijethubutu kurudia makosa na kuwa yeye alikuwa chadema na hana wajua kuwa ni wababaishaji kwa maslahi yao na si maslahi ya umma..
    Paul Makonda alizungumzia juu ya umuhimu wa serikali tatu,,na makosa ya UKAWA kutoka nje akiwataka warudi bungeni kama kweli wao hawalipwi na mawakala wao wa nje ya nchi ili wakae nje ya bunge.
    mkt Kibwana akiongea kuwakilisha vijana wa Zanznibar aliwaaambia wana Mbeya KUWA ;"muungano hudumu daima na kuwa ukiona Mzanzibar anapinga muungano huu wa serikali mbili basi wajue huyo ni hamnazo na analake jambo"






  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.