Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

December 31, 2015

  • TAARIFA YA UTAPELI


    TAARIFA YA UTAPELI



  • December 30, 2015

  • Spika wa Bunge, Job Ndugai Arejea Kutoka India


    Spika wa Bunge, Job Ndugai Arejea Kutoka India
    Ndugai (1)Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu.

    Ndugai                (2)Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishai na Madini Mhe. Medard Kalemani mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambula na aliyeko kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.NdugaiKatibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumpokea katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu. Katikati ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson.

    Spika wa bunge, Job Ndugai amerejea leo kutoka india alikokuwa ameenda kwa ajili ya matibabu. Awashukuru Watanzania kwa maombi yao. Aelezea hali yake kuwa ni imara kabisa.


  • WAZIRI WA FEDHA AFICHUA MAZITO JUU YA SAFARI ZA KWENDA KUOMBA MSAADA NCHI ZA NNJE


    WAZIRI WA FEDHA AFICHUA MAZITO JUU YA SAFARI ZA KWENDA KUOMBA MSAADA NCHI ZA NNJE

    Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amesema serikali inatarajia kukusanya kiasi cha Sh. trilioni 1.3 ndani ya mwezi huu pekee.


    Aidha, amesema ili kuhakikisha serikali inapata mapato ya kutosha, atasimamia vyema suala la kukusanya kodi zinazostahili na kutengeneza mazingira ya watu kulipa kodi.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kuapishwa, Dk. Mpango alisema kwa kipindi cha mwezi mmoja serikali inaweza kukusanya kiasi hicho cha fedha.

    "Nimekaa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kipindi cha wiki tatu, nimeona kuwa kiasi hiki cha Sh. trilioni 1.3 kinaweza kukusanywa. Kwa wiki iliyopita ya sikukuu, niliona makusanyo ni mazuri na mpaka ifikapo mwisho wa mwezi huu, tutatimiza kiasi hicho," alisema.


    Namna ya kukuza Uchumi wa Nchi
    Dk. Mpango, alisema ili kukuza uchumi wa nchi ni lazima kuwa na utaratibu wa kujenga viwanda vikubwa nchini vinavyozalisha kwa wingi  jambo litakaloongeza pato la taifa.

    "Nchini kwa sasa kuna kiwanda kimoja kikubwa cha Bia cha Breweries (TBL) ambacho ndicho tunakitegemea ndio maana bei ya vileo vinapanda kila siku. Lakini vingekuwapo kama hivyo 10, nina uhakikisha tungekusanya mapato ya kutosha," alisema.

     Aibu ya kuomba misaada nje
    Dk. Mpango, alisema miongoni mwa mambo yanayomnyima raha ni safari za kwenda ughaibuni kuomba misaada kwa nchi wahisani.

    Alisema kitendo hicho ni cha aibu na kwa muda mrefu kimekuwa kikimsonesha moyoni hasa kwa kuwa anafahamu kuwa taifa lake lina utajiri mkubwa.

    "Nimekwenda nje mara nyingi nikiongozana na mawaziri wa fedha waliopita kwenda kuomba misaada.Huwa najisikia aibu sana,tunadhalilika sana. 
     
    "Hatuna sababu ya kuwa ombaomba,tunachotakiwa kukifanya ni kuimarisha mfumo wa ukusanyaji kodi na kuwaondolea mzigo wananchi wa hali ya chini," Alisema Dr. Mpango


  • BREAKING NEWZZ: SERIKALI YA MAGUFULI KIBOKO, KIGOGO MWINGINE ASIMAMISHWA KAZI LEO


    BREAKING NEWZZ: SERIKALI YA MAGUFULI KIBOKO, KIGOGO MWINGINE ASIMAMISHWA KAZI LEO


    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    OFISI YA RAIS








    Anuani ya Simu "TAMISEMI" DODOMA
    Simu Na: (026) 2322848, 2321607,
    2322853, 2322420,
    Nukushi: (026) 2322116, 2322146.
    2321013,
    Barua pepe:ps@poralg.go.tz

    Tawala za Mikoa
    na Serikali za Mitaa,
    S. L. P. 1923, DODOMA.
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu fisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.
    Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.
    Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
    Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.
    Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.
    Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.


    Imetolewa na:
    Rebecca Kwandu
    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
    Ofisi ya Rais - TAMISEMI


  • WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI KIGOMA



    WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI KIGOMA
    maj2
    * Ni ubadhirifu wa fedha za umma, atoa siku mbili kukamilisha uchunguzi
    * Ataka apewe taarifa ya maandishi Januari Mosi, 2016
    WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Eng. John Ndunguru kukamilisha uchunguzi wake na kumpatia taarifa ya maandishi juu ya tuhuma ubadhirifu wa fedha za umma unaohusisha uuzwaji wa jengo la KIGODECO na viwanja 12 vya Manispaa 
    ya Kigoma/Ujiji ambao unadaiwa kukiuka taratibu.

    Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Desemba 30, 2015) kwenye ukumbi wa NSSF, mjini Kigoma wakati akizungumza na viongozi na watendaji mbalimbali wa mkoa huo alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku mbili mkonai humo.
    Waziri Mkuu Majaliwa amesema anazo taarifa kuwa jengo hilo liliuzwa kwa sh. milioni 370/- pamoja na jengo jingine la MIBOS kwa sh. milioni 50/- licha ya kupewa barua na Mkuu wa Mkoa huo kusitisha uuzwaji wa jengo pamoja viwanja hivyo, bado liliuzwa.
    "Katibu Tawala wa Mkoa kaa na Mkurugenzi wa Manispaa, Mhandisi wa Manispaa na Mhasibu na unipatie taarifa kwa maandishi ifikapo Jumamosi hii," alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
    "Nataka kujua nani alifanya tathmini ya jengo, ni kwa nini jengo liliuzwa kwa thamani hiyo, je ndiyo thamani halisi ya jengo? Ni kwa nini RC alipozuia, utaratibu uliendelea? Je, utaratibu wa uuzaji ulifuatwa? Ni kwa nini viwanja viliuzwa chini ya thamani,? Katibu Tawala kaa na watu wako na uniletee hiyo taarifa kwa maandishi. Tukigundua kuna mianyamianya tutachukua hatua za kinidhamu," alisema.
    Viongozi walioagizwa kukutana na Katibu Tawala wa Mkoa ni Mkurugenzi wa Manispaa, Eng. Boniface Nyambele; Mhandisi wa Manispaa, Eng. Boniface William na Mhasibu wa Mapato wa Manispaa, Ndg. Bawili Mkoko.
    Kuhusu uuzwaji wa jengo na viwanja, imebainika kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Luteni Kanali (Mst), Issa Machibya alizuia uuzaji huo kwa barua ya tarehe 16 Juni 2015 akitaka viwanja hivyo vitumike kwa matumizi ya manispaa na mchakato huo usitishwe hadi mwakani lakini agizo lake lilipuuzwa na jengo likauzwa kwa sh. milioni 370 ambayo ni bei ya kiwanja pekee.
    Tuhuma nyingine zinazopaswa kuchunguzwa ni pamoja na matumizi ya sh. milioni 809 kwa ajili ya ujenzi wa maabara. Kiasi hicho kilitolewa kutoka kwenye fedha za miradi ya maendeleo (Capital Development Grants-CDG), Mradi wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifugo (ASDP), Mradi wa Uendelezaji Miji (Tanzania Strategic Cities Programme –TSCP) na Miradi ya Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (SEDP).
    Inadaiwa kwamba Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa idara ya mipango na fedha walitumia ujenzi wa maabara kama kigezo cha kuchota fedha hizo bila kutoa taarifa kwa wakuu wa idara husika ambao walikasimiwa fedha hizo.
    Tuhuma nyingine ni manunuzi hewa ya vipuri (spare parts) vyenye thamani ya sh. milioni 8 na manunuzi hewa ya stationeries yenye thamani ya sh. milioni 4.6/-. Haya yanadaiwa kufanywa Julai 25, mwaka huu na Mkurugenzi huyo akishirikiana na Mhasibu Mkoko.
    Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam mchana huu.


  • RUNGU ZITO;KAMPUNI 5 ZA SIMU NCHINI ZAPEWA ADHABU KALI NA TCRA,KISA HIKI HAPA ....!!!!



    RUNGU ZITO;KAMPUNI 5 ZA SIMU NCHINI ZAPEWA ADHABU KALI NA TCRA,KISA HIKI HAPA ....!!!!
     
     
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

    HATUA ZA KISHERIA NA KIUDHIBITI KWA MAKAMPUNI YA SIMU YALIYOSHINDWA KULINDA WATEJA WAKE KITEKNOLOJIA NA KISHERIA KUHAKIKISHA USALAMA WA MAWASILIANO YAO

    1. Katika shughuili zake za udhibiti wa huduma za mawasiliano nchini, Mamlaka ya Mawasilaino Tanzania imepokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya kuwepo mazingira yasiyo salama katika huduma za mawasiliano na hivyo kusababisha kufanyika kwa vitendo vya utapeli unaofanywa kwa kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai, hivyo kusababisha watu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

     Kwa mfano kupokea ujumbe kutoka namba unayoifahamu ukikuagiza utume fedha au ujumbe wa kashfa au matusi wakati hautoki kwa mhusika mwenye namba. Mamlaka imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja na malalamiko mengine hupelekwa Polisi. Kwa miezi miwili tu, matukio 42 yameripotiwa Polisi pamoja na TCRA ambayo tukio moja tu linakuwa na ulaghai wa takribani milioni 25 peke yake.

    2. Tarehe 16 Oktoba, 2015 Mamlaka iliwakumbusha watoa huduma za simu nchini juu ya wajibu wao kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya utumaji wa jumbe za kilaghai na kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai. 

    Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mamlaka tarehe 16 Desemba, 2015 Mamlaka ilibaini kuwa  kampuni za Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart), MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo), Airtel Tanzania Limited, Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel) and Zanzibar Telecom Limited inayojulikana kama Zantel) zimeshindwa, zimepuuzia na zimekataa kufuata maagizo ya Mamlaka kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za kilaghai kinyume na Kanuni Na.8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011].

    3. Tarehe 18 Disemba, 2015 Mamlaka iliwaamuru watoa huduma za mawasiliano waliotajwa hapo juu kufika mbele ya Mamlaka na kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao kwa kuvunja sheria na kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya Mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweka mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

    4. Watoa huduma walifika na kutoa maelezo ya utetezi kati ya tarehe 21 na 23 Desemba, 2015.

    5. Baada ya kuwasikiliza na kutilia maanani utetezi wa watoa huduma na kwa mujibu wa uchunguzi na majaribio uliofanywa na Mamlaka, Mamlaka imejiridhisha kuwa mitandao ya watoa huduma waliotajwa hapo juu haikuwa salama na kuwa watoa huduma hao walishindwa kufuata maelekezo ya Mamlaka juu ya kuweka mazingira salama katika huduma wanazotoa. 

    Hivyo Mamlaka imejiridhisha kuwa watoa huduma wamekiuka matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya mwaka 2011 (The Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011) inayowataka watoa huduma kuweka mazingira ya mitandao salama kwa kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na utumaji wa jumbe za kilaghai kupitia mitandao yao.

    6. Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Jedwali la Pili katika Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria za Nchi, kinachoipa Mamlaka uwezo wa kutoa adhabu kwa Wenye Leseni dhidi ya uvunjifu wa Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni, Mamlaka ya Mawasiliano imetoa:

    A. Onyo kali kwa Kampuni za:
    (i) Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart),
    (ii)  MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo),
    (iii)  Airtel Tanzania Limited,
    (iv)  Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel), na
    (v) Zanzibar Telecom Limited (inayojulikana kama Zantel).

    kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Postal ya mwaka 2011  [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweza mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

    B. Imeamuru Kila Kampuni husika:
    (i)   Kuhakikisha kuwa, kuanzia siku ya kutolewa kwa amri hii, inaweka mazingira salama katika mtandao wake yatakayozuia utumaji wa jumbe za kilaghai (yaani 'spoofed messages') na matishio mengine ya kiusalama;
    (ii)   Kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Tano (Shs 25,000,000.00) kwa Mamlaka ya Mawasiliano kabla ya tarehe 29 Januari, 2016; na
    (iii) Endapo Makamuni haya yatashindwa kutimiza amri Na.2 hapo juu, Mamlaka itachukua hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya Kampuni ya Simu husika.

    7. Aidha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapeda kuchukua fursa hii kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na jumbe za kuwataka kutuma fedha bila ya kuwa na uhakika. Inashauriwa kuhakiki ujumbe husika kwa kupiga simu na kuongea na mhusika kabla ya kufanya maamuzi ya kutuma fedha hata kama namba inayotumika unaijua. 

    Vilevile wawe makini wanapopokea jumbe zinazoonesha zinatoka kwa mtu fulani wanayemjua kumbe ni matapeli wanaotumia ulaghai kwa njia hii ya "spoofing".

    IMETOLEWA NA
    Dkt. Ally Y. Simba
    MKURUGENZI MKUU
    30 Disemba, 2015


  • WAZIRI TAMISEMI AMWAGIZA MKURUGENZI KUTUMBIA JIPU HILI MARA MOJA



    WAZIRI TAMISEMI AMWAGIZA MKURUGENZI KUTUMBIA JIPU HILI MARA MOJA
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na  Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

    Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.

    Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

    Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha  Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.

    Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.

    Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

    Imetolewa na:
    Rebecca Kwandu
    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
    Ofisi ya Rais - TAMISEMI


  • December 26, 2015

  • HIVI NDIVYO POLISI WALIVYOYAKAMATA KIULAINI MAGUNIA HAYA YA BANGI



    HIVI NDIVYO POLISI WALIVYOYAKAMATA KIULAINI MAGUNIA HAYA YA BANGI
    Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kukamata magunia sita ya Bangi baada ya kutelekezwa na wamiliki walipoona askari polisi waliokuwa katika doria.


    Akiongea na waandishi wa habari jana katika kituo kidogo cha polisi cha Lamadi wilayani Busega kamanda wa polisi mkoani Simiyu Germini Mushy amesema.
     
    Amesema kuwa magunia hayo sita yenye uzito wa kilo 269 yalikamatwa kufuatia msako huo huku wamiliki wake watatu wakiyakimbia na kuacha baiskeli zao walipoona polisi.
     
    Aidha katika tukio lingine kamanda Mushy amesema kuwa mnamo disemba 22, mwaka huu majira ya saa 9 alasiri gari lenye namba T 366 VCJ kampuni ya J4 lilikutwa na begi likiwa na mirungi yenye uzito wa kilo 20 ndani yake.


  • Waraghabishi wakoleza kasi ya mabadiliko wilayani Kishapu


    Waraghabishi wakoleza kasi ya mabadiliko wilayani Kishapu
    Watendaji wa Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbele ya jengo la kituo hicho likiwa limekamilika kutokana na michango yao ya fedha na nguvu kazi. 


    Na Krantz Mwantepele ,Kishapu 

    Mabadiliko katika jamii yoyote kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ongezeo la mahitaji ya binadamu katika mambo mbalimbali. Kwamba, kadri dunia inavyopitia mabadiliko, kadiri ile ile changamoto, mahitaji na huduma katika jamii husika huongezeka.

    Ili kufikia malengo yanayotokana na misukumo na mageuzi yasiyokwepeka, binadamu amelazimika kubuni mikakati mbalimbali ya maendeleo. Si hivyo tu, mabadiliko haya yamemfungulia binadamu fursa ya uthubutu wa kujaribu mambo mbalimbali, siyo tu kwa faida yake, bali jamii nzima inayomzunguka.

    "Sikutegemea kama siku moja katika maisha yangu nitapata wazo ambalo lingebadili na kushawishi watu kuchukua hatua kwa mustakabali wa jamii." 

    Hiyo ni kauli ya mraghbishi Revocatus Richard ambaye pia, kitaaluma ni mwalimu katika shule ya msingi Uchunga. Richard alitoa kauli hiyo baada ya kupitia mafunzo ya uraghbishi na mwalimu mwenzake, Restusta Katobesi, ambao baadaye kwa pamoja, walianzisha Kituo cha KIMAJU (Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga) kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na wananchi. Na hilo ndiyo lilifanya achaguliwe kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho. 

    Walimu hao walikuwa miongoni mwa waraghbishi 30 walioshiriki mafunzo ya uraghbishi yaliyotolewa mwezi Machi, mwaka 2012 wilayani Kishapu katika mkoa wa Shinyanga. Kutokana na faida na maarifa waliyoyapata kwenye mafunzo hayo, walimu hao waliamua kuunda umoja uliokuwa chachu ya kuanzishwa kituo hicho cha maendeleo.

    Mwanazuoni Sarah Earl, aliwahi kusema: "Maendeleo ni watu na mazingira yao. Kwamba, kusingekuwa na maana iwapo barabara, hospitali, shule na miradi mingine ya maendeleo inayojengwa kwa ajili ya watu isingetumika." 

    Kwa mantiki hiyo, miradi yote ya maendeleo, ikiwamo Chukua Hatua ni kwa ajili ya ustawi wa maisha ya watu. Kwa kuwa kiini cha maendeleo ni watu. Shabaha kubwa ya mradi huu wa Chukua Hatua ni kuhakikisha wananchi (waraghbishi) wanajielewa na kujitambua katika kutimiza majukumu yao na kupata haki zao zikiwamo huduma bora za kijamii na kuhakikisha wananufaika na rasilimali zao. Pia unawasaidia kuwawajibisha viongozi wao ili watimize majukumu yao ya kuhamasisha maendeleo na kutatua shida za wananchi.

    Mraghbishi ni mwananchi anayeleta uhai mpya ndani ya jamii kwa kutambua matatizo na kupendekeza njia sahihi za kuyatatua.Katika kipindi cha miaka mitano ya mradi, zaidi ya waraghbishi 380 wameleta uhai katika jamii zao, hususani kwenye vijiji vya mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Arusha hasa katika wilaya ya Ngorongoro.

    Tafsiri ya uhai huu ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wabadhirifu, watendaji wabovu, kuandaa midahalo, kudai huduma bora za kijamii, kuibua na kufuatilia matatizo mbalimbali katika vijiji vyao kama ambavyo waraghbishaji Richard na Katobesi wamefanya.

    Uraghbishi Kijiji cha Uchunga 

    Baada ya kupatiwa mafunzo ya uraghbishi, walimu hawa walirudi kijijini kwao wakiwa na jukumu moja la kutambua changamoto zinazoikabili jamii yao na kupendekeza nini kifanyike wakitumia nafasi na uwezo walio nao.

    Kikubwa walichoangalia ni mustakabali wa mtoto wa Kijiji cha Uchunga, kwa maana ya nafasi ya mtoto, ikiwamo ya kufahamu huduma anazopata.Katika kufikiria sehemu ya kuanzia na ili kumpa mtoto wa kike nafasi katika jamii, hasa ya kuongoza, walianza na wanafunzi wa shule wanayofundisha, Uchunga.

    "Nimepata bahati ya kuwa mwalimu mkuu msaidizi mara kadhaa na nimetumia fursa hiyo kuleta mabadiliko, nikianzia kubadilisha utaratibu wa kuchagua viongozi wa wanafunzi katika shule yetu," alisema Richard na kuongeza:

    "Kwanza tulibadilisha wazo la Kaka Mkuu na badala yake tukasema tutakuwa na Kiranja Mkuu, ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa kike kushika nafasi za uongozi wa wanafunzi."

    Hadi sasa chaguzi mbili za kidemokrasia za kuchagua viongozi wa wanafunzi zimefanyika shuleni Uchunga Julai 2012 na Mei 2013. 

    Katika kuhakikisha wanaendeleza mawazo hayo, waraghbishi hao walikuja na wazo la kujenga kituo cha kujisomea. Walianza kuwatembelea wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Uchunga wanaoishi katika kijijini hapo. 
    Baadhi ya wananchi na wajumbe wa Kituo cha Maendeleo cha Uchunga wakiwa mbele ya kituo kabla hakijaezekwa na mabati.

    Ili kufikia malengo yao, waliomba ushirikiano, siyo tu kwa walengwa ambao ni wanafunzi, bali kutoka kada zingine ndani ya jamii.

    Akielezea jinsi walivyoanza, mraghbishi Katobesi alisema:

    "Tulikutana na wanafunzi na kuunda umoja wa kikundi wa Wanafunzi wa Sekondari Uchunga (UWASU). Kikundi hiki kiliamsha hamasa kwa wanafunzi waliokukubali kujitolea kufanya kazi." 

    Na baadhi ya wanafunzi hao wametembelea shule nyingine na kuhamasisha wenzao kujitolea kusaidia kazi mbalimbali kama kuchota maji na kuokota mawe kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kituo hicho cha kujisomea. 

    Ndani ya jamii yoyote kuna mamlaka, hivyo ili malengo yao yatimie kuliwalazimu waraghbishaji hao kupata ruhusa kutoka kwa walimu na aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji wakati huo, Mahona Punguja.

    "Baada ya kutoka kwenye mafunzo yao, walikuja kuzungumza na mimi kuhusiana na mambo waliyojifunza na jinsi watakavyoleta mabadiliko. Nilikubaliana nao na kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wazazi kama wadau muhimu na makundi mengine maalumu," alisema Punguja.

    Makundi maalumu ni pamoja na watumishi wa uma, kwa maana ya walimu na mtendaji wa kijiji na kata, wazee maarufu, viongozi wa dini, vijana na wajumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji. Waraghbishi hawa kwa ushirikiano na uliokuwa uongozi wa serikali ya kijiji waliweza kukutana na makundi hayo ili kuwaelimisha kuhusu wazo la kituo cha kujisomea. Baada ya kila kundi kukutana na waraghbishi, uliitishwa mkutano wa pamoja wa kujadili jambo hilo na kamati ikaundwa ya kusimamia mchakato mzima. Kamati hii ilichaguliwa kwa kila kundi kuwa na mwakilishi wake. 

    "Njia ya kwanza ilikuwa ni kukusanya fedha, kisha kuwaomba wananchi kuchangia nguvu zao. Kila mmoja kwa nafasi yake alijitolea. Wengine tulisomba mawe na kuchimba msingi. Wanawake walileta vyakula kwa ajili ya mafundi ambao nao walijitolea pia utaalamu wao bure", anaelezea Michael Butu, Mwenyekiti wa Kituo cha KIMAJU.

    Wanajamii waliohamasika waliombwa kuchangia kila mmoja Shilingi 10,000 za Kitanzania, ingawa baadhi walitoa nusu ya mchango huo. Kila kitongoji kiliombwa kuchangia Shilingi 60,000. Michango hii ilikusanywa baada ya kuundwa kwa nguvu ya pamoja na wenyeviti wa vitongoji. Kati ya vitongoji vitatu, viwili vilikamilisha ahadi zao.

    Harakati hizi ziliwezesha wanajamii kujenga kituo hadi ngazi ya linta, kabla ya mlezi wa kituo hicho, Charles Dida kutoa shilingi 355,000 kama mkopo kwa ajili ya kununua mabati na mbao. 

    "Nilipoona jengo letu linasuasua, niliamua kujitolea kufanikisha ujenzi. Niliamua kumshirikisha mke wangu, ambaye aliunga mkono uamuzi wangu kwa kujua mafanikio yatakayopatikana ni ya jamii nzima," alisema Charles Dida.

    Katika hili tumejifunza mahusiano yaliyopo baina ya baba na mama katika kufanya maamuzi ya pamoja. Ni tofauti na mfumo dume uliozoeleka katika jamiii ya kisukuma. Na mpaka sasa kituo kimeweza kulipa kiasi cha Shilingi 110,000 na hivyo bado kinadaiwa Shilingi 245,000. 

    Ili kuhakikisha kituo kinaendelea kutoa huduma kwa watoto wa Uchunga wajumbe wa kamati tendaji wanafanyakazi kwa kujitolea kwa kuwa wao kuwa sehemu ya jamii ya wananchi wa kijiji cha Uchunga. 

    "Nilihamasika baada ya kupendezwa na wazo la kuanzishwa kwa kituo hiki. Na siku nilipoombwa kuwa sehemu ya kuleta mafanikio, nilikubali mara moja na kushiriki mikutano na ratiba nyingine," alifafanua katibu wa vijana, Bahati Juma.

    Moja ya majukumu aliyokabidhiwa ni huhakikisha kituo kinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. Kwa wastani, kituo kinahudumia wanafunzi 20 kwa siku. 

    Mbali na katibu huyo, watendaji wengine ni pamoja na mkurugenzi, katibu, mhasibu, na kamati tendaji chini ya mwenyekiti na mlezi wa Kituo. Nafasi hizi zote zina wasaidizi isipokuwa ya mkurugenzi na mlezi.

    Uongozi huu ulipatikana kidemokrasia kwa kuchaguliwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Baada ya kupata uongozi walitengeneza katiba na kukisajili kituo chao. Kwa mujibu wa katiba ya kituo hicho, uongozi unachaguliwa kila baada ya miaka mitatu. 

    "Waasisi wa kituo ndio waliopendekeza mfumo wa uongozi na baada ya hapo wakauwakilisha kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Kwa hiyo walioweza walishiriki. Na kila mtu aliyeona anafaa kuwa sehemu ya uongozi wa kituo hicho alipendekeza jina lake ama la mwenzake. Baada ya majina hayo kupatikana ndipo yalipigiwa kura na kupata viongozi," anafafanua mwenyekiti wa kituo, Michael Butu. 

    Tukiachilia suala la uongozi, kuna utaratibu maalumu wa kuendesha kituo hicho. Kuna vijana wanaohusika na kuhakikissha ofisi inafunguliwa ili kutoa huduma za kujisoma bure, ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha watu na kukifahamu kituo.

    Huduma za KIMAJU

    Taasisi hii ya kijamii kwa kiasi kikubwa imelenga kwenye uzalishaji maarifa kwa kutoa huduma ya maktaba, ambayo wanafunzi wanaoishi kijiji cha Uchunga hutumia kusoma na kufanya kazi za nyumbani baada ya masomo shuleni.

    Katika ziara za ufuatiliaji na uwezeshaji, wafanyakazi wa shirika mtendaji la TAMASHA katika mradi huo wa Chukua Hatua, walishauri kituo kupanua wigo wa huduma zake, kama anavyoelezea Afisa Mradi Winston Churchill.

    "Tuliwashauri kuwalenga pia vijana walio nje ya shule ili kuwawezesha vijana wote kutumia kituo hicho vizuri kijijini hapo."

    Watu wazima pia wanatumia kituo hicho kujisomea magazeti, ambayo huwa ni ya siku nyingi na hii ndio sababu ya umuhimu wa kutafuta redio ili watu wasikilize taarifa za habari. 

    Hali hii imehamasisha wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kuja kujisomea, kama anavyoelezea mwanafunzi wa darasa la saba Leticia Isaka kutoka Shule ya Msingi Uchunga,
    "Kituo kinanisaidia kutambua mambo mbalimbali, kwa mfano kupitia mafunzo ya hapa, napata malezi bora ya kuniandaa niwe mwalimu au daktari. Lakini si hivyo tu, wakati wa mapumziko ya saa sita huwa tunakuja kujisomea hapa baada ya kupatiwa mazoezi na walimu shuleni," 

    Pamoja na sababu nyingine, uwepo wa kituo hiki umechangia kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu katika shule ya sekondari ya kata ya Uchunga, ambapo mwaka 2013 jumla ya wanafunzi .... tu ndio waliofaulu katika ngazi ya ... , wakati mwaka uliofuata waliongezeka na kufikia kiasi cha ...

    "Mbali na mafanikio haya, kituo kina changamoto kadhaa ikiwamo ukosefu wa meza, viti na makabati ya kuhifadhia vitabu," anasema mkurugenzi wa kituo, Richard na kuongeza:

    "Haya mabenchi na meza tumeazima kanisani na tukimaliza tunarudisha sehemu husika. Hatuna vitabu vya mitaala kwa ajili ya wanafunzi wetu, ingawa eneo la kujisomea lipo vizuri, nishati ya umeme nayo ni shida." 

    Kimsingi, wanajamii wa Uchunga kwa kushirikiana na waraghbishi na uongozi kwa kijiji wamefanikiwa kufikia malengo.



  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.