February 27, 2016

  • MTOTO ALIYETENGENEZA JEZI YA LIONEL MESSI KWA MFUKO WA PLASTIKI, ATUMIWA JEZI HALISI NA NYOTA HUYO



    MTOTO ALIYETENGENEZA JEZI YA LIONEL MESSI KWA MFUKO WA PLASTIKI, ATUMIWA JEZI HALISI NA NYOTA HUYO
    Mtoto wa kiume mwenye uraia wa taifa la Afghanistan ambaye hivi karibuni aligonga vichwa vya mitandao ya kijamii kwa ku vaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Argentina.

    160225110545__88438940_messi_boy

    Murtaza wa Afghan akivalia jezi nzuri aliyotumiwa na Messi

    BBC ilimsaidia Messi kumtafuta mtoto huyo ambaye anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa Argentina. Murtaza Ahmadi mwenye miaka 5, anatoka katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

    Timu ya usimamizi wa Messi ilithibitisha siku ya Alhamisi kwamba Murtaza alitumiwa jezi ya mshambuliaji huyo wa Argentina iliotiwa saini pamoja na mpira kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona.

    "Ninampenda Messi na fulana yangu inasema Messi ananipenda,"Murtaza alisema,tayari akimuigiza mshambuliaji huyo anavyosheherekea bao lake.
    Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na picha moja iliyoenea katika mitandao ikimuonyesha amevaa fulana ya plastiki ya Messi.

    160127133410_afgha_boy_messi_640x360_twitterjoynaw5

    Hii ndio jezi aliyotengeza nyumbani na kuvaa

    Source: BBC


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.