July 21, 2014

  • SALAMU ZA POLE WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


    SALAMU ZA POLE WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
    Uongozi na Wafanyakazi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki unatoa pole kwa Katibu Mkuu wake Bi. Joyce K.G. Mapunjokufuatia kifo cha Mume wake Profesa Zakaria Mmbwambo (58) kilichotokea Jumamosi tarehe 19 Julai 2014, Dar es Salaam.
    Wizara inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kuipa mkono wa pole familia ya Profesa Mmbwambo katika kipindi hiki kigumu.
    Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe

    Imetolewa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

    21 Julai 2014


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.