Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Philipp Lahm amestaafu kucheza soka la kimataifa, baada ya kukiongoza kikosi chake na kushinda Kombe la Dunia nchini Brazil.Beki huyo wa Bayern Munich, ambaye pia anaweza kucheza kama kiungo, ameichezea Ujerumani mara 113.Lahm, 30, ataendelea kucheza Bayern Munich, ambapo amesaini mkataba hadi mwaka
2018. Habari za kustaafu kwake kuichezea timu ya taifa zimethibitishwa na chama cha soka cha Ujerumani DFB.
Lahm alianza kuichezea Ujerumani Februari 2004 walipoichapa Croatia 2-1, na amestaafu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia.
0 comments:
Post a Comment