July 07, 2014

  • Al-Shabab washambulia tena Kenya na kuua watu 29 wasio na hatia



    Al-Shabab washambulia tena Kenya na kuua watu 29 wasio na hatia
    Watu 29 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya watu wenye silaha za moto kufanya mashambulizi mawili katika eneo la Lamu, Pwani ya Kenya, Jumamosi (July 5).

    Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa watu hao waliokuwa na silaha nzito walivamia kituo cha biashara katika kijiji cha Hindi, Lamu na pia Kituo cha Polisi cha Gamba Jumamosi usiku.

    Shambulizi hilo liliwalenga wananchi wasio na hatia na kuharibu magari na nyumba.

    Kundi la kigaidi la Al-Shabab limedai kuhusika moja kwa moja na mauaji hayo kwa sabababu za kulipiza kisasi kwa kuwa wanajeshi wa Kenya wanalisaka kundi hilo nchini Somalia.

    Kundi hilo lilidai kuhusika pia na mashabulizi mengine yaliyofanyika awali kwa sababu kama hizo.

    Jumapili, July 6, Makamo wa rais wa Kenya, William Ruto alilitembelea maeneo yaliyoshambuliwa..
    Funny Quote of the Day
    If you can't convince them, confuse them.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.