Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri wa Kilimo Maendeleo ya chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza, na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Lindi wakati akitembelea katika Mabanda ya Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo Mkoa wa Lindi, jan Agosti 8, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Kilwa Murtaza Mangungu, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Ngongo katika maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana Agosti 8, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Jarida la Kilimo la Nanenane kutoka kwa Iman Kajula, kwa ajili ya kuzinduliwa wakati wa Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana Agosti, 8, 2014.
0 comments:
Post a Comment