July 01, 2014

  • RAIS WA URUGUAY ALIVYOWALINGANISHA FIFA NA WATOTO WA MBWA …kisa? adhabu ya Suarez

     

    Fury: Jose Mujica has called FIFA 'a bunch of old sons of b*****s' in an attack on football's governing body

    RAIS wa Uruguay Jose Mujica (pichani) amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa'' au "a bunch of old sons of bitches".

    Hii ni baada ya maafisa wa shirikisho hilo kumfungia kwa miezi minne mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez.

    Suarez alipata adhabu hiyo ambayo inasemekana kuwa kali sana kuwahi kutolewa katika hoistoria ya kombe la dunia kwa kumuua mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.

    Rais Mujica anasifika kwa kutotafuna maneno yake pamoja na ukali wa matamshi yake.

    Aliyatoa matamshi yake kupitia televishini ya taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kubanduliwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika hatua ya mtoano raundi ya pili.

    Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa kile alichosema, lakini wandishi wa habari tayari walikuwa wamemrekodi. Lakini hata hivyo alitoa ruksa ya kuyachapisha matamshi yake pale alipoulizwa na waandishi hao iwapo alitaka kujirekebisha.

    Rais huyo alisema kuwa FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge.

    Pia alitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa sana kwa historia ya FIFA.

    Hata hivyo wakati Rais wa Uruguay anaikoromea FIFA, Suarez amemuomba radhi Giorgio Chiellini kupitia ukurusa wake wa Twitter hali inayoonyesha kuwa amekubali na kujutia makosa yake.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.