
Jeshi nchini Nigeria linasema limewakamata wanawake              watatu ambao walikua wanawaandikisha wafuasi wanawake kwa              kundi la siasa kali za Kiislamu la Boko Haram.
        Inadaiwa wanawake hao waliwalenga wajane na              wasichana wadogo wakiwaahidi kuwachumbia kwa wafuasi wa Boko              Haram.
        Mwaandishi                wa BBC Will Ross akiwa Abuja anasema inaelekea Boko Haram                inajaribu kuwashawishi wanawake washiriki vilivyo katika                mapambano yao.
        Mwezi uliopita mshambuliaji mwanamke wa kujitoa              mhanga alifariki alipojaribu kuishambulia kambo ya kijeshi              katika jimbo la Gombe - tukio la kwanza aina hiyo nchini              Nigeria.
        Bomu hilo lililipuka alipokua            akipekuliwa katika kituo cha usalama . Mwanajeshi mmoja pia            aliuwawa.
        Wanawake pia ni miongoni mwa wale waliokamatwa na              kuzuiliwa katika miji ya Maiduguri kaskazini mwa Nigeria,              eneo ambalo Boko Haram wanaungwa mkono kiasi .
        Jeshi la Nigeria limesema wanawake watatu              iliowakamata walikuwa ni wa tawi la upelelezi.
        Ilisemekana mmoja wao alikua ni mjane wa mpiganaji              wa Boko Haram.
        Kundi hilo la wanaharakati wa Kiislamu bado              linawashikilia zaidi ya wasichana wa shule 200 iliowakamata              mnamo mwezi wa Aprili katika mji wa Chibok katika jimbo la              Borno .
        Boko Haram inadai wapiganaji wake na jamaa zao              waachiliwe kwa kubadilishana na wasichana.Serikali              imelikataa dai hilo
         
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment