July 12, 2014

  • FIFA YATANGAZA WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA



    FIFA YATANGAZA WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA
    Fifa imetangaza orodha ya majina 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia - 2014 Golden Ball.
    Wachezaji watatu wametoka Argentina, Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi. Mahasimu wao wa siku ya Jumapili Ujerumani, imetoa wachezaji wanne, Mats Hummels, Toni Kroos, Phillip Lahm na Thomas Muller.
    Wengine ni James Rodriguez kutoka Colombia, Neymar wa Brazil na Arjen Robben wa Uholanzi.
    Fifa pia imetangaza majina ya watakaowania tuzo ya golikipa bora wa michuano hiyo. Keylor Navas wa Costa Rica, Manuel Neuer wa Ujerumani na Sergio Romero wa Argentina watawania tuzo hiyo.
    Wakati huohuo Memphis Depay wa Uholanzi, Paul Pogba na Raphael Varane wa Ufaransa wamechaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika Kombe la Dunia.
    Washindi watatangazwa baada ya mchezo wa fainali siku ya Jumapili





  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.