July 01, 2014

  • FEYENOORD YAKIRI BEKI WAKE STEFAN DE VRIJ YUKO NJIANI KUTUA MANCHESTER UNITED

     

    On his way: Feyenoord believe Stefan de Vrij is destined for Manchester United in the coming weeks

    KLABU ya Feyenoord ya Holland inaamini kuwa safari ya mchezaji wake Stefan de Vrij kutua Old Trafford itakamilika wiki chache zijazo.

    Timu hiyo imejiweka tayari kumkosa beki huyo wa kati na tayari imeanza kuangalia mbadala wa nyota huyo wa miaka 22 anayeshiriki kombe la dunia na kikosi cha timu ya taifa ya Holland huko nchini Brazil.

    Vrij anaonekana atakataa ofa ya kujiunga na Lazio na badala yake dhamira yake ameielekeza United chini ya kocha Van Gaal kwa ada inayokisiwa kuwa ni pauni milioni 7.

    Kocha wa Feyenoord, Fred Rutten amesema: "Nilisaini mkataba wa kuitumikia Feyenoord kwa mazingira yoyote yale. Kama mchezaji anaondoka, hupaswi kuomboleza. Nina imani tutakuwa na nafasi nzuri ya kuziba mapengo."

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.