January 14, 2015

  • SIMBA WAREJEA DAR NA KOMBE LA MAPINDUZI



    SIMBA WAREJEA DAR NA KOMBE LA MAPINDUZI
    Golikipa chipukizi wa Timu ya Simba Sc,Manyika Peter 'Manyika Jr' (wa pili kushoto) wakiwakabidhi Kombe Mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kuwasili kutokea visiwani Zanzibar kwenye Mashindano ya Mapinduzi Cup,ambapo Simba waliibuka mabingwa.
    Mashabiki wa timu Simba SC wakishangilia ubingwa wao.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

    Na Bakari  Issa ,Globu ya Jamii Dar

    Klabu ya Soka ya Simba leo hii imerejea jijini Dar es Salaam toka visiwani Zanzibar ambapo imeibuka kinara wa Kombe la Mapinduzi jana Januari13 katika mchezo uliopigwa usiku katika uwanja wa Amaan.

    Akizungumza  mara baada ya kuwasiri jijini Dar es Salaam,Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Klabu ya Simba,Juma Ngambili amesema  vijana wamewapa  mashabiki wao kitu wanachokitaka licha ya kupata ushindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 4-3 na kusema kuwa mashabiki wasubiri mambo mazuri toka kwao.

    "Tumeupokea ushindi kwa mikono miwili,na tumewapa wapenzi wetu kitu wanachotaka na tunawasihi mashabiki wasubiri mambo mazuri toka kwetu,"alisema Ngambili

    Aidha,Ngambili amewatoa hofu mashabiki wa Klabu ya Simba katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na kuwaambia kuwa watakuwa vizuri kwa kuanzia na mchezo unaowakabili siku ya Jumamosi dhidi ya Ndanda.

    Kwa upande wake nahodha wa Simba,Nassor Masoud 'Chollo' amesema mchezo wao wa fainali dhidi yao na Mtibwa Sugar ulikuwa mgumu na kusema kuwa fainali ni fainali licha ya kuibuka na ushindi.Naye,Golikipa chipukizi wa Klabu hiyo,Manyika Peter 'Manyika Jr' amesema siri ya mafanikio yakwake na ya Klabu ni kujituma zaidi na amewaomba mashabiki wa Simba kuiunga mkono klabu yao.

    "Katika mchezo wa jana nilitolewa kwenye dakika ya 90 naamini kama Kocha angeniacha nidake mikwaju ya penalti ningedaka,tumenyakua Kombe la Mapinduzi kutokana na wachezaji tulijituma na nawasihi mashabiki wetu kutuunga mkono. 


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.