Mmoja wa majeruhi wa shambulio la                      leo akipatiwa huduma ya kwanza na kikosi cha                      uokoaji.
                              POLISI mmoja wa kike                ameuawa kwa risasi huku wafagiaji wa mitaani wakijeruhiwa                baada ya kushambuliwa na mtu aliyekuwa na silaha katika                shambulio la pili ndani ya saa 24 lililotokea eneo la                Montrouge jijini Paris nchini Ufaransa.
          Shambulio la leo                limetokea kusini mwa mji wa Paris huku mshambuliaji                aliyekuwa amaevaa nguo ya kuzuia risasi 'bullet prof'                akitumia silaha aina ya M5.
          Polisi huyo alisimaa mtaani                  kukagua ajali iliyotokea barabarani kabla ya                  kushambuliwa na mtu huyo.
          Shuhuda wa shambulio hilo                  anadai kusikia milio ya risasi tano kwenye tukio hilo.
          Shambulio                hilo limetokea ndani ya saa 24 baada ya shambulio la jana                katika ofisi za magazeti ya vikatuni ya Charlie Hebdo                jijini Paris, Ufaransa lililoua watu 12 na kujeruhi                kadhaa. Bado haijafahamika kama shambulio la leo lina                uhusiano wowote na lile la jana.
        
0 comments:
Post a Comment