January 16, 2015

  • WATUHUMIWA WA ESCROW WATATU WAFIKISHWA KIZIMBANI LEO


    WATUHUMIWA WA ESCROW WATATU WAFIKISHWA KIZIMBANI LEO
    Baadhi ya watuhumiwa wa Escrow wakipandishwa mahakamani.
    MZIMU wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, limeendelea kuwatafuna watuhumiwa  wa uchotwaji wa  mabilioni ya fedha za akaunti hiyo baada ya watuhumiwa wengine watatu kupandishwa mchana huu kizimbani katika mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

    Waliopandishwa  ni Meneja  wa Misamaha ya Kodi  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) Leonard Mutabingwa  ambaye anadaiwa kupokea rushwa ya zaidi ya  shilingi bilioni moja kama zawadi kutoka kwa Rugemalira, Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Mkombozi , Julius Ruta, ambaye anadaiwa kupokea zaidi ya shilingi milioni 100  pamoja na  Ofisa Mwandamizi wa Tanesco, Steven Urasa,   anayetuhumiwa kupokea  zaidi ya shilingi milioni 100.

    Mpaka tunatoka mahakamani hapo ni mtuhumiwa mmoja tu aliyefanikiwa kuwa nje kwa dhamana ya kuweka nusu ya fedha anazotuhumiwa kupokea akitakiwa kuwa na watu wawili kama wadhamini.  Watuhumiwa wengine walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na  kesi zao kutajwa tena tarehe  27, 29 Januari na 11 Februari mwaka huu.

    bofya play video hapa chini

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.