Hospitali ya rufaa              Bugando iliyopo jijini mwanza imepunguza gharama za upasuaji              wa moyo, kutoka kati ya shilingi milioni tatu hadi nane              ilizokuwa inawatoza wagonjwa kwa upasuaji mkubwa na mdogo              hadi kufikia shilingi elfu hamsini tu ili kuwawezesha              wananchi wengi wasio na uwezo wa kumudu gharama hizo              kunufaika na matibabu hayo.
            
                        
        Mkuu wa idara ya upasuaji wa moyo na                kifua katika hospitali ya rufaa Bugando Prof. William                Mahalu amessema kutokana na ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa                moyo, zaidi ya watoto 20 wanaopata huduma ya kliniki                katika hospitali hiyo pamoja na watu wazima 25 wamekuwa                kila mwezi wakigundulika kusumbuliwa na tatizo la moyo,                ambapo mwaka huu watoto 10 wamegundulika na tatizo hilo na                watoto sita wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka.
            Daktari bingwa wa kitengo cha                upasuaji wa moyo kwa watoto katika hospitali hiyo Dk.                Godwin Sharau pamoja na kuzishukuru taasisi za nje ya                nchi, wadau na marafiki wa hospitali ya rufaa Bugando                waliosaidia operesheni za moyo kufanikiwa kwa gharama                nafuu kabisa, amesema mwaka huu lengo ni kuwafanyia                operesheni wagonjwa 100 na miaka mitatu ijayo ni kufikia                wagonjwa 250 kwa mwaka.
            Mkuu wa wilaya ya Kwimba Selemani                Mzee amesema huduma hiyo inayofanywa na idara ya upasuaji                wa moyo na kifua inapaswa kuwafikia wananchi wengi                hususani wa vijijini ambao pamoja na kusumbuliwa na tatizo                hilo lakini wanahofia gharama kubwa ya matibabu, huku                mzazi wa mtoto Lukaiya Shaban Bw. Shaban Juma Ramadhan                ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa moyo na madaktari                bingwa wa magonjwa ya moyo katika hospitali hiyo                akishukuru kwa huduma hiyo.
            Upasuaji wa moyo katika hospitali ya                rufaa Bugando ulianza miaka saba iliyopita, ambapo hadi                kufikia mwaka jana 2014, hospitali hiyo ilikuwa na jumla                ya wagonjwa 769 waliokuwa wakingoja kufanyiwa upasuaji,                aidha katika kipindi hicho watoto 44 walipelekwa Israel,                38 walitibiwa katika hospitali hiyo – ambapo 14                walifanyiwa upasuaji na madakatari bingwa wa moyo kutoka                Australia na wengine 24 walifanyiwa upasuaji na timu ya                madakatari wa hospitali ya Bugando.
          
0 comments:
Post a Comment