Mratibu wa kituo cha              TFGM na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure              ya Kijiji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara,              Thomas Maruga akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo              na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na              mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa              (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi wa              Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu              duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa              sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu              wa ukeketaji (Waiseke wa Kisasa).(Picha za Zainul Mzige wa              MOblog)
        .Na              Mwandishi wetu, Tarime-Mara
        SERIKALI              imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa              mabinti wa koo za Kikuria nchini.
        Kauli              hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na              ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika              akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa              sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu              wa ukeketaji.
        Alisema              jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili              yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala ya afya na              kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.
        Aidha              wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
        Alisema              adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika              kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha              Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la kuendeleza mila.
        "Hii              sio mila" anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna              mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha              mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima              ipigwe vita.
                Mgeni rasmi Waziri              wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka (wa pili kushoto)              akiwasili kwenye mahafali hayo pamoja na Mratibu Mkazi wa              mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la              Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro              Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Shirika              la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani              (UNFPA), Dkt Natalia Kanem.
        Alisema              serikali isiache kuwatetea mabinti hao kwa dai la kuwa hiyo              ni mila kwa kuwa wanaofanyiwa vitendo hivyo hulazimishwa na              haifanyiki kwa ridhaa yao.
        Alisema              wapo mabinti walioletwa na wazazi wao kuepushwa na janga              hilo, wapo waliotoroka kwa wazazi wao na wapo walioletwa              katika kituo hicho na polisi kutoka makwao.
        Mafunzo              hayo ya mwezi mmoja yamelenga kukabiliana na msimu wa              ukeketaji ambao sisita huyo alisema mwaka jana ulianza              mapema Novemba na unaendelea hadi mwaka huu wakati kimila              mwaka huu si wa ukeketaji.
        Kwa              mujibu wa mila za Kikuria ukeketaji hufanyika katika mwaka              unaogawanyika, mwaka 2015 haugawanyiki.
                Mhashamu Askofu Mkuu              wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara, Michael              Msongazila akiwasili kwenye sherehe za mahafali ya sita ya              kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga wilayani Tarime              mkoani Mara.
        Mafunzo              hayo ambayo yamelenga kuwatoa mabinti wa kisasa wenye              mwelekeo wa maisha yenye hali bora mabinti wanaofika hapo              huwa hawataki kukeketwa na ndio maana mwaka huu walipata              tatizo la binti mmoja kuzimia wakati alipomuona baba yake              katika maeneo ya kituo hicho.
        Alisema              wapo wazazi wakorofi wanaokuja kudai watoto wao lakini pia              ipo jamii korofi inayotumia ubabe baada ya wasichana hao              kutoka hapo wanakeketwa kwa lazima.
        Katika              hafla hiyo iliyoendeshwa na masista wa shirika la Daughters              of Charity of St. Vincent De Paul, Waziri wa Kazi na Ajira              Mh. Gaudentia Kabaka aliwapongeza wasichana hao na kuwataka              kuwa mfano katika jamii na kutekeleza wajibu wao.
        Alisema              wamekuwa mabinti wa kisasa kwa kukataa ukeketaji na hivyo              wao wanastahili kuwa walimu kwa wenzao.
                Maandamano ya              wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure iliyopo              kijiji cha Masanga wilayani Tarime, mkoani Mara wakiwa na              mabango yenye jumbe mbalimbali za kukemea ukeketeji              wakisindikiza dada zao wahitimu wa kituo cha FGMT katika              sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti (Waiseke wa kisasa)              waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji yaliyofanyika mwanzoni mwa              wiki.
        Aidha              Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi              wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,              Alvaro Rodriguez amewataka mabinti hao kuwa chachu ya              mabadiliko katika jamii na kuwa chanzo cha kubadili kizazi              kijacho.
        Alisema              wamesimama madhubuti kupinga mila potofu na uonevu na kusema              kwa kitendo chao wamewafanya wengine kuwaiga na kubadilika.
        Alisema              ukeketaji ni mila potofu na kusema kwa msaada wa shirika la              Umoja wa mataifa la Mpango wa familia (UNFPA) na taasisi              nyingine zinazopambana na ukeketaji kwa kipindi cha miaka              saba wamefanikiwa kuwoakoa wasichana 2001 wasikeketwe.
        Aidha              mabinti hao wameokolewa dhidi ya ndoa za utotoni, ujauzito              wa mapema na kushindwa kuendelea na masomo.
                Naye              Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia              Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem amesema ni              vyema mapambano dhidi ya ukeketaji yakaendelea kwa kuwa              wanaoshabikia ni viongozi wa kimila na ngumu kuiondoa ila              kwa juhudi za jamii yenyewe.
        Katika              sherehe hizo ambapo pia askofu wa Musoma alikuwepo na              viongozi wengine wa kiserikali pia Ngariba walioacha kazi              hiyo walikuwepo kuelezea ubaya wa mila hiyo.
         Suala              la ukeketaji ni kitu cha kawaida katika mikoa ya Manyara              71%, Dodoma 64%, Arusha 57%, Singida 51% na Mara 40%.
        Viongozi              waliopata muda wa kuzungumza walisema kwamba ukeketaji              unatakiwa kukomeshwa mara moja kwani ni tatizo si tu kwa              jamii bali kwa wale ambao wanafanyiwa kisaikolojia na              kitabibu.
                Wahitimu mabinti 37              waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji wa kituo cha TFGM cha              kijiji cha Masanga wakiwasili na maandamano kwenye sherehe              za mahafali ya sita ya kituo hicho.
        Moja ya              kazi inayoifanywa na kituo cha Masanga ni ushauri wa              kisaikolojia kutokana na wasichana wengi kufika hapo wakiwa              na matatizo makubwa ya magonjwa na hasa msongo wa mawazo.
        Katika              risala yao mabinti hao wameitaka serikali kufanyakazi yake              kukabiliana na ubabe unaofanywa na viongozi wa kimila wa              kuwalazimisha kukeketwa hata msimu unapokuwa umepita.
        Mabinti              hao ambao wengi wametoka shule ya msingi na sekondari              wameweza kuwekwa hapo kwa msaada wa UNFPA ambao wametoa hela              kupitia Children's Dignity Fund (CDF), .Wafadhili wengine ni              Daughters of Charity of St. Vincent Du Paul, na Askofu wa              kanisa katoliki dayosisi ya Musoma, Michael Msongazila
                Mgeni rasmi Waziri              wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akisalimiana na              Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma              Mkoani Mara, Michael Msongazila mara baada ya kuwasili              kwenye mahafali hayo.
                Kwaya ya vijana ya              mara ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za              mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga              wilayani Tarime mkoani Mara.
                Mgeni rasmi Mh.              Kabaka, Bw. Alvaro Rodriguez na SSP. Simon Mrashani              wakishiriki kucheza wimbo maalum unaohamasisha kukataza              vitendo vya uovu vya Ukeketaji kwa watoto wa kike wakati wa              mahafali hayo.
                Meza kuu ikitoa              heshima kwa wimbo wa taifa.
                Mkurugenzi wa Kituo              cha kupambana na ukeketaji cha Masanga (TFGM), Tarime,              mkoani Mara, Sista Germaine Baibika akimkaribisha mgeni              rasmi pamoja wageni waalikwa kwenye sherehe ya mahafali ya              sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
                Mgeni rasmi Waziri              wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akifurahi jambo na              Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi              wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,              Alvaro Rodriguez kwenye sherehe za mahafali hayo.
                Mgeni rasmi Waziri              wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akizungumza kwenye              sherehe za mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu              wa ukeketaji.
                Mratibu Mkazi wa              mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la              Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro              Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe              za mahafali sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa              ukeketaji.
                Mkuu wa Wilaya ya              Tarime, mkoani Mara, Bw. John Henjewele akitoa salamu kwa              niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika mahafali ya sita ya              kituo cha kupambana na ukeketaji cha kijiji cha Masanga              (TFGM) cha wilayani Tarime, mkoani Mara.
                Mwakilishi wa              Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu              duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem, akizungumza kwenye              sherehe hizo.
                Kaimu kamanda wa              polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya SSP. Simon              Mrashani akieleza jinsi jeshi la polisi linavyoshiriki              katika kupambana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia              likiwemo suala la kesi za ukeketaji ambapo pia alitoa              takwimu za kesi zilizoripotiwa kituoni mpaka sasa ni 141,              huku 80 zikiwa Mahakamani na 20 zimetolewa hukumu.
                Mtaalam wa Mahusiano              na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu              akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa              sherehe za mahafali hayo.
                Wahitimu 37 wakila              kiapo cha kutokubali kutoshiriki kukeketwa na kuwa mabalozi              wazuri kwenye jamii zao katika kuelemisha madhara ya              ukeketaji kwa wanaoendeleza mila na tamaduni hizo pindi              warudipo majumbani. Kwa picha zaidi ingia              humu
        
0 comments:
Post a Comment