Watu wasiojulikana wamelichoma moto na kuliteketeza Kanisa la Evangelical Assemblies of God wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma na kuteketekeza kila kitu kilichokuwemo ndani ya kanisa hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto                  amesema kuwa tukio hilo la mwanzoni mwa wiki hii,                  limeacha athari kubwa za mali na kwamba hakuna mtu                  yeyote ambaye amepata madhara kuhusiana na uharibifu.
            Mwamoto ambaye ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya                  Kakonko, alisema kuwa bado haijajulikana hasa sababu ya                  kuchomwa kwa kanisa hilo.
            Lakini, alibainisha kuwa sababu mbili kubwa,                  ikiwemo ya mgawanyiko wa viongozi na masuala ya kisiasa                  yanaweza kuwa chanzo cha tatizo hilo.
            Alisema zipo taarifa za masuala ya kisiasa                  kufanywa na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo, ikiwemo                  vyombo vilivyokuwa vinatumika kwenye kampeni kwa mgombea                  wa  uenyekiti wa kijiji hicho kupitia chama cha NCCR –                  Mageuzi, ambaye ni kiongozi wa kanisa na ambaye                  alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kijiji.
            Alisema kuwa masuala hayo ya siasa na mgogoro wa                  viongozi wa kanisa, yanafanyiwa kazi kwa kina ili                  kubaini ukweli.
            Alisema kwamba kiongozi mmoja wa kanisa hilo,                  anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama akituhumiwa                  kuhusiana na uchomaji huo .
            Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Jafari                  Mohammed alithibitisha tukio  hilo na kwamba uchunguzi                  kujua sababu hasa za kuchomwa kwa kanisa hilo,                  unaendelea.
          
0 comments:
Post a Comment