Mke wa Rais Mama Salma Kikwete            akisalimiana na Josephine Kulea kutoka Taasisi ya Samburu            Girls ya nchini Kenya mara baada ya binti huyo kutoa ushuhuda            wake kuhusu namna alivyoathirika na ndoa za utotoni wakati wa            mkutano wa Marais na Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika kuhusu            kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni uliofanyika huko Addis            Ababa nchini Ethiopia tarehe 29.1.2015. Binti huyo alijifungua            mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17.
        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete            akisalimiana na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama            Ban Soon Taek wakati wa mkutano wa Marais na Wakuu wa Nchi za            Afrika uliozungumzia kampeni ya kupiga vita ndoa za utotoni            barani Afrika wakati wa kikao cha 24 cha Umoja huo            kilichofanyika Addis Ababa tarehe 29.1.2015.
        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete            akisalimiana na Mke wa Rais wa Chad na Mwenyekiti wa Umoja wa            Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) Mama Hinda            Deby Itno  wakati wa kikao kilichoandaliwa na Jumuia ya Afrika            kuzungumzia kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani humo            tarehe 29.1.2015.
        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete            akizungumza na Mke wa Rais wa Niger Mama Malika Issoufou            Mahamadou mara baada ya kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika            kuhusu kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani humo.
        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete            akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Malawi Mama Gertrude            Maseko Mutharika(wa kwanza kulia) pamoja na Mama Ban Soon            Taek, Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (katikati) wakati            wa kikao cha Wakuu wa nchi za AU kinachofanyika mjini Addis            Ababa tarehe 29.1.2015.
        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete            akisalimiana na Mama Margaret Kenyatta mara baada ya            kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika kilichozungumzia kampeni            ya kutokomeza ndoa za utotoni.
        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa            katika picha ya pamoja na wake wa Marais na Wakuu wa nchi za            Afrika mara baada ya kikao cha kampeni ya kutokomeza ndoa za            utotoni barani Afrika. Wengine katika picha ni (kutoka kushoto            kwenda kulia), Mama Ban Soon Taek, Mke wa Katiubu Mkuu wa            Umoja wa Mataifa, Mama Widad Babker, Mke wa Rais wa Sudan,            Mama Salma Kikwete, Mama Hinda Deby Itno. Mke wa Rais wa Chad            (mwenye begi mkononi), Mama Esther Lungu, Mke wa Rais wa            Zambia, Mama Hadidja Aboubaker, Mke wa Rais wa Comoro, Mama            Roman Tesfaye, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mama            MalikaIssoufou, Mke wa Rais wa Niger, Mama Margret Kenyetta na            Mwisho ni Mama Gertrude Mutharika, Mke wa Rais wa Malawi.
        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete            akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa            mkutano wa kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani            Afrika. Wengine katika picha ni Mama Widad Babker ,Mke wa Rais            nwa Sudan, Mama Esther Lungu, Mke wa Rais wa Zambia na Mama            Margaret Kenyatta.
        PICHA          NA JOHN LUKUWI
        







0 comments:
Post a Comment