Askari wa jeshi lapolisi,              Sajenti Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi akiwa              katika ofisi yake kwenye ghala lakuhifadhia silaha katika              kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi mkoani mbeya.
        Akizungumza na Paparazi              wetu kwanjia ya simu, kamanda wa polisi mkoawambeya amekiri              kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha kifo hicho              bado hakijafahamika na kwamba jeshi lapolisi linaendelea na              uchunguzi wa tukiohilo.
        Sajenti Patrick mwenye              umri wamiaka 54 ,akiwa katika ofisi yake kwenye chumba cha              kuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya              mbozi amejipiga risasi mdomoni ambayo imetokea kisogoni na              kuondoka na uhai wake, tukio ambalo limetokea majira ya saa              tisa usiku na kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya              ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ambaye pia ni mkuu wa              wilaya ya ileje, Rosemary Staki Senyamule.
        Baadhi ya waombolezaji              ambao wamezungumza na Mwandishi wetu wamesema kuwa wamepokea              msiba huo kwa masikitikomakubwa hasa kwa kuzingatia kuwa              Sajenti Patrick alikuwani askari mwadilifu na anayeipenda              kazi yake.
        
0 comments:
Post a Comment