Kamanda wa polisi wa          mkoa wa ruvuma ACP Mihayo Msikhela  amethibitisha kutokea kwa          tukio hilo na kusema chanzo cha tukio hilo ni Wafanyabiashara          hao kudhulumiana fedha za biashara za mbao walizopata.
        Kamanda mihayo amesema          kuwa marehemu ameacha ujumbe  wa kurasa nne unaoeleza sababu ya          yeye kuua na kisha kujiua.
        Katika ujumbe wake          kamanda mihayo anasema marehemu moshi ametaja fedha alizokuwa          akimdai mtu aliyemuua kiasi cha shilingi milioni  87  na Pia          marehemu moshi  ameandika namba zake  za simu  kwa mawasiliano          katika bahasha aliyowekea ujumbe huo.
        
0 comments:
Post a Comment