Katibu Mkuu wa Umoja wa                Mataifa, Ban Ki Moon pamoja na washiriki wa hafla ya                kuwakumbuka walinzi wa amani wakisimama kwa dakika moja                kuwaenzi walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu                ambao ni wafanyakazi wa umoja wa mataifa waliopoteza                maisha wakati wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea                nchini Haiti mwaka 2010 na wale ambao wamepoteza maisha                kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014.
                    Ban Ki Moon akizungumza                wakati wa hafla hiyo ambayo iliibua hisia na majonzi                makubwa miongoni wa washiriki wa hafla hiyo ya kuwaenzi                walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu                waliopoteza maisha wakati wakitekeleza wajibu wao wa                kuwasaidia wananchi waliokuwa matatizoni. Miongoni mwa                wahanga hao waliokumbukwa katika hafla hiyo ni Mashuja                Watatu Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ)                waliopoteza maisha wakati wakitimiza wajibu wao katika                Misheni ya Kulinda Amani ya MONUSCO katika Jamhuri ya                Kidemokraria ya Kongo. Mashujaa hao ni Luteni Rajabu                Mlima, Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian                Msigila
                    Mwakilishi wa Kudumu wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,                Balozi Tuvako Manongi akitoa heshima zake mbele ya mshumaa                mkubwa ambao uliandaliwa kama ishara ya kuwakumbuka na                kuwaenzi Walinzi wa Amani na Watoa Misaada ya kibinadamu                waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao katika                kipindi cha tetemeko la aridhi lililotokea mwaka 2010 huko                Haiti na wale waliopoteza maisha kati ya Octoba 2013 na                Novemba 2014. katika kipindi hicho Tanzania ilipoteza                mashujaa wake watatu waliokuwa wakihudumu katika Misheni                ya MONUSCO huko DRC
          Na Mwandishi Maalum
            Umoja wa Mataifa jana Alhamisi                  umewakumbuka walinzi wa Amani   na  wafanyakazi ya umoja                  wa mataifa waliopoteza maisha wakati wakitekeleza                  majukumu yako katika kipindi cha Octoba 2013 na November                  2014.
             Kumbukumbuka hiyo  imefanyika  katika                  siku  kama ya jana ( January 8) miaka mitano iliyopita                   palitokea   tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti na                   kupoteza  maisha ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo                   pamoja  na  uhalibifu  mkubwa wa  mali ilivuta hisia za                  waliohudhuria hata baadhi yao kutokwa na machozi
            Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki                   Moon akizungumza katika hafla hiyo amesema,                   anasikitishwa sana na  ongezeko  la mashambulizi                  yanayofanywa  dhidi ya walinzi wa Amani pamoja na                  watoaji wa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi                  wa  mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
            Jumla ya  wahanga 102 walipoteza maisha                  nchi Haiti   wakati lilipotokea tetemeko hilo mwaka                  2010,  huku wengine 100 walipoteza maisha kati ya Octoba                  2013 na Novemba 2014. Wahanga hao  ni walinzi wa Amani                  na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa  kutoka mataifa                  mbalimbali duniani  na walikuwa wakihudumu katika                  Misheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa  na Mashirika                  yake.
            Kati ya   waliokumbukwa jana wapo                  walinzi wa Amani watatu kutoka Jamhuri ya Muungano wa                  Tanzania ambao walipoteza maisha huko  Jamhuri ya                  Kidemokrasia ya Kongo walikokuwa wakihudumu katika                  Misheni ya MONUSCO.
            Mashujaa hao wa kitanzania   na ambao                  majina yao yalisomwa moja  baada ya jingine sambamba na                   mashujaa wenzao wengine. Ni Luteni Rajabu  Mlima,                   Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian                  Msigila.
            Ban Ki Moon amesema   walinzi  wa Amani                  na watoaji wa misaada ya kibinadamu wamekuwa wakipoteza                  maisha katika mazingira ambayo ukiacha yale yatokanayo                  ya majanga asili yakiwamo magonjwa ya milipuko na ajali,                  wengine wamepoteza maisha kwa mashambulizi yanayofanywa                  kwa makusudi. 
            Na kwa sababu hiyo Katibu Mkuu anasema,                   Umoja wa Mataifa unaendelea na jitihada zake za                  kuimarisha   ulinzi wao    ikiwa ni  pamoja na                  kuwajengea mazingira salama ya utendaji kazi  yakiwamo                   mafunzo na vifaa 
            Ameongeza kuwa  ushirikiano na michango                  kutoka nchi wanachama wa umoja wa mataifa ni  muhimu                  sana  hasa katika kipindi hiki ambapo siyo tu pamekuwapo                  na ongezeko kubwa la mahitaji ya walinzi wa Amani na                  watoaji wa misaada ya kibinadamu, lakini pia kutokana na                  ongezeko la  mashambulizi  dhidi yao na mazingira magumu                  ya kazi.
          
0 comments:
Post a Comment