Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

January 30, 2015

  • MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA KAMPENI YA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI BARANI AFRIKA.‏


    MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA KAMPENI YA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI BARANI AFRIKA.‏

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Josephine Kulea kutoka Taasisi ya Samburu Girls ya nchini Kenya mara baada ya binti huyo kutoa ushuhuda wake kuhusu namna alivyoathirika na ndoa za utotoni wakati wa mkutano wa Marais na Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika kuhusu kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni uliofanyika huko Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 29.1.2015. Binti huyo alijifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17.



    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama Ban Soon Taek wakati wa mkutano wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika uliozungumzia kampeni ya kupiga vita ndoa za utotoni barani Afrika wakati wa kikao cha 24 cha Umoja huo kilichofanyika Addis Ababa tarehe 29.1.2015.

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Chad na Mwenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) Mama Hinda Deby Itno  wakati wa kikao kilichoandaliwa na Jumuia ya Afrika kuzungumzia kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani humo tarehe 29.1.2015.

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Niger Mama Malika Issoufou Mahamadou mara baada ya kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika kuhusu kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani humo.

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Malawi Mama Gertrude Maseko Mutharika(wa kwanza kulia) pamoja na Mama Ban Soon Taek, Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (katikati) wakati wa kikao cha Wakuu wa nchi za AU kinachofanyika mjini Addis Ababa tarehe 29.1.2015.

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Margaret Kenyatta mara baada ya kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika kilichozungumzia kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni.

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika mara baada ya kikao cha kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani Afrika. Wengine katika picha ni (kutoka kushoto kwenda kulia), Mama Ban Soon Taek, Mke wa Katiubu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mama Widad Babker, Mke wa Rais wa Sudan, Mama Salma Kikwete, Mama Hinda Deby Itno. Mke wa Rais wa Chad (mwenye begi mkononi), Mama Esther Lungu, Mke wa Rais wa Zambia, Mama Hadidja Aboubaker, Mke wa Rais wa Comoro, Mama Roman Tesfaye, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mama MalikaIssoufou, Mke wa Rais wa Niger, Mama Margret Kenyetta na Mwisho ni Mama Gertrude Mutharika, Mke wa Rais wa Malawi.

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni barani Afrika. Wengine katika picha ni Mama Widad Babker ,Mke wa Rais nwa Sudan, Mama Esther Lungu, Mke wa Rais wa Zambia na Mama Margaret Kenyatta.

    PICHA NA JOHN LUKUWI


  • Mh.Mbatia: Jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake



    Mh.Mbatia: Jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake
    Serikali imeshauriwa jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake ambao kwa sasa unalalamikiwa kwa sehemu kubwa na wananchi kwa kukiuka haki za binadamu.

    Akizungumza jana mjini Dodoma katika kuhitimisha hoja kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa wa chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama wake,Mbatia alisema kuwa kitendo hicho kilikiuka haki za binadamu ikiwemo wanawake kudhalilishwa kijinsia.

    Mh. Mbatia emeongeza kuwa ili chaguzi zijazo ziwe za amani na utulivu ameishauri serikali kubadilisha sera za vyama vya siasa na utawala pamoja na mfumo wa jeshi la polisi kuendeleza amani na utulivu ambavyo kwa sasa vinaonekana kuanza kutoweka.

  • SIKU YA KWANZA MAZOEZINI KWA KINDA WA REAL MADRID MARTIN ODEGAARD


    SIKU YA KWANZA MAZOEZINI KWA KINDA WA REAL MADRID MARTIN ODEGAARD

    Martin Odegaard and Gareth Bale set off during a sprint              exercise at Real Madrid training on Thursday

    Kinda wa Norway Martin Odegaard aliingizwa moja kwa moja kwenye kikosi cha wakubwa katika siku yake ya kwanza ya mazoezi ya Real Madrid aliyojiunga nayo hivi karibuni.

    Dogo huyo wa miaka 16 mwenye kipaji cha hali ya juu cha kutandaza soka, alionekana pichani akiwa sambamba na Gareth Bale katika zoezi la kukimbia Alhamisi asubuhi kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

    The Wales forward opens up his legs as he strides away              from the teenager, who joined the club last week

    Bale uses his explosive power to burst away from              Odegaard during the sprint exercise

    Bale alionekana akimhenyesha Odegaard kabla ya baadae kumpa maneno ya kumjenga huku akimkumbatia begeni.

    Bale was spotted offering some words of encouragement              to Odegaard as he put his arm around his shoulder

    Odegaard anategemewa kumalizia sehemu ya msimu iliyobakia akiwa na timu B lakini siku zote atakuwa akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza chini ya kocha Ancelotti.

    Norway international Odegaard insists he signed for              Real Madrid for sporting reasons, not financial

    The 16-year-old, who signed a £40,000 per week              contract, listens on during the session on Thursday morning



  • January 29, 2015

  • Z’BAR WASHINDWA KUNUNUA NDEGE ZA VIONGOZI



    Z'BAR WASHINDWA KUNUNUA NDEGE ZA VIONGOZI
    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema kuwa haina ubavu wa kununua ndege kwa matumizi ya viongozi wake.
    Waziri wa Fedha Zanzibar, Omary Yussuf Mzee alisema hayo jana alipojibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Muyuni, Jaku Hashim Ayoub katika kikao cha Baraza la Wawakilishi.
    Alisema mpango huo unaweza kufanikiwa baada ya Zanzibar kuanza kuchimba nishati ya mafuta na gesi.
    Alisema SMZ itaendelea kukodi ndege kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya matumizi ya viongozi wake.
    Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kuwa gharama za uendeshaji wa ndege za Serikali ya Muungano wa Tanzania hutolewa na Serikali ya Muungano, hivyo SMZ hulazimika kukodi na kulipia gharama.
    "Kuiweka ndege moja Zanzibar ili itumike kwa viongozi wetu wa kitaifa ni jambo linalowezekana, lakini kufanya hivyo ni kuongeza gharama za uendeshaji, kwani wakala watalazimika kuweka vifaa na wataalamu wa kuzihudumia ndege hizo," alisema Waziri Mzee.
    Awali, mwakilishi huyo alitaka kufahamu gharama za matumizi ya ndege za Serikali ikiwamo Foker 50 na 25 zinapotoa huduma SMZ kama zinalipwa na Serikali ya Muungano au wahisani.
    Pia, mwakilishi huyo alitaka kujua kwa nini ndege moja isiwe na maskani yake Zanzibar badala ya kutumika visiwani humo na Tanzania Bara.


  • January 26, 2015

  • THE MAGAZETI YA BONGO LEO MONDAY /JUMATATU 26/1/2015 LIVE!!



    THE MAGAZETI YA BONGO LEO MONDAY /JUMATATU 26/1/2015 LIVE!!
    .


    .
    .
    .
    .
    .
    DSC08694
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    DSC08688
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    .
    Ni


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.