Kioo cha lori cha mbele kikiwa kimepasuka.
WATU watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya Coca Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu, mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia ghafla mbele ya gari hilo kubwa lililokuwa limebeba vinywaji na ndipo gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu.
(Habari/Picha na: Gabriel Ng'osha/GPL)
0 comments:
Post a Comment