August 06, 2014

  • WAKUU WA IDARA ZINAZOHUSIKA NA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE WATAKIWA KUWAPA VIPAUMBELE WAKULIMA WADOGO WADOGO



    WAKUU WA IDARA ZINAZOHUSIKA NA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE WATAKIWA KUWAPA VIPAUMBELE WAKULIMA WADOGO WADOGO






    WAKUU wa Idara zinazohusika na maonesho ya wakulima ya nanenane wametakiwa kuwapa vipaumbele wakulima wadogo wadogo badala ya shughuli zote kufanywa na wao.
    Wito huo  ulitolewa jana na Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Wakulima Tanzania(MVIWATA), Hasira Zahoro,alipokuwa akizungumza na gazeti hili baada  ya kutembelea banda la Mviwata katika maonesho ya Wakulima nanenane yanayoendelea jijini Mbeya.
    Alisema katika mabanda ya Halmashauri nyingi waoneshaji wakubwa sio wakulima bali ni maafisa kilimo, mifugo na uvuvi hivyo hawampi nafasi Mkulima mdogo wa kujifunza.
    Alitolea mfano banda la Mviwata ambalo linawaoneshaji 18 ambao wote ni wakulima wadogo wakiongozwa na mwezeshaji mmoja na kufanya banda kuwa la wakulima moja kwa moja kwa kuwa ndiyo walengwa wa shughuli za nanenane.
    Alisema katika banda la Mviwata wanaotembelea watapata fursa ya kujifunza mambo mbali mbali ya kilimo na ufugaji kutoka kwa wakulima wenyewe baada ya kufundishwa na kuyanyia kazi mafunzo mbali mbali.
    Zahoro alisema lengo la maonesho ya mwaka huu ni kuimarisha mawasiliano na kuwaunganisha wakulima wadogo kupitia vikundi na mitandao yao katika ngazi mbali mbali ili kujenga mtandao wa kitaifa wenye nguvu.
    Alisema mtandao huo ukiunganishwa utawawezesha kuwa na ushiriki na uwakilishi wa ukweli wa maslahi ya wakulima wadogo katika ngazi zote za maamuzi.
    Aliongeza kuwa wananchi mbali mbali wakitembelea banda la Mviwata wataweza kujifunza jinsi masoko ya wakulima yanavyofanya kazi, maswala ya kuweka na kukopa, tiba asili na bidhaa mbali mbali za wakulima.
    Na Mbeya yetu



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.