October 06, 2014

  • EID KUBWA YA KIHISTORIA LEICESTER



    EID KUBWA YA KIHISTORIA LEICESTER

    Wanajumuia wa An Noor Leicester pamoja na ndugu na marafiki kutoka ndani ya mji huo na mingine ya Uingereza kama vile London, Leeds na Coventry Jumamosi tarehe 4 Oktoba walijumuika kusherehea sikukuu ya Eid Ul Adh-ha katika Masjid An Noor, Belgrave Gate.
    Ilikuwa ni sherehe ya kihistoria, ambayo ilianza kwa Takbeer kisha Sala ya Eid, na kufuatiwa na Khutba iliyotolewa na Imamu Mkuu Sheikh Saleh Juma.
    Kabla ya waumini kukumbatiana na kupongezana, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jumuia ya An Noor Sheikh Mohammed Omar alisimama na kutoa taarifa ya kihistoria, kwamba Jumuia imefanikiwa kwa uwezo wa Allah, kutimiza lengo lake la kununua jengo inalolikodi, hapo 170a Belgrave Gate Leicester. ALLAHU AKBAR!
    Mwenyekiti akaarifu kuwa Jumuia imefanikiwa kukusanya kiwango cha kutosha kulipa £175,000 kwa ajili ya kukamilisha manunuzi. Pia imekusanya pesa zaidi kuweza kununua kiwanja nyuma ya jengo kinachomilikiwa na Halmashauri ya jiji la Leicester ili kupanua zaidi ukubwa wa jengo. 
    Mwenyekiti akawashukuru wote wanaotoa michango yao, na akaomba waumini wasiache kuendeleza misaada yao kwani kazi inayofuata ni kubwa zaidi.
    Baada ya hapo ndipo Waumini wakapata nafasi ya kupongezana, na hatimaye wote, wake kwa waume, wakaketi kujipatia kifungua kinywa kwa pamoja.
    Kullu Am wa Antum Bikhayr!


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.