August 07, 2014

  • WAKULIMA, WAJASILIAMALI, WAFANYABIASHARA WANAFUNZI NA WATU MBALIMBALI WANUFAIKA NA MAFUNZO BURE YALIYOTOLEWA NA BENKI YA NMB NANE NANE MBEYA



    WAKULIMA, WAJASILIAMALI, WAFANYABIASHARA WANAFUNZI NA WATU MBALIMBALI WANUFAIKA NA MAFUNZO BURE YALIYOTOLEWA NA BENKI YA NMB NANE NANE MBEYA
     Mtoa Mafunzo kutoka  Benki ya NMB Rodgers Shipela wa kwanza kulia akitoa mafunzo ya kina kwa waliohudhuria semina hiyo juu ya Elimu ya Kibenki kwa ujumla lakini pia kubwa alitoa mafunzo ya Jinsi ya Kuanza Biashara na kuiendeleza, kutoa  mafunzo ya jinsi ya kujua kufanya ushindani katika biashara, pia alitoa mafunzo kwa vyama vya ushirika juu ya utawala bora na jinsi wanavyoweza kuviendesha kwa usahihi kabisa, zaidi alitoa elimu juu ya wajasiliamali wakulima na wafanyabiashara wanavyoweza kuweka pesa zao na kuzitunza .

     Alex Masawe wa kwanza Kulia akitoa mafunzo kwa wajasilamali, wakulima,wafanyabiashara pamoja na watu wengine waliofika katika mafunzo, hapa akielezea juu ya utayarishaji wa mipango ya kibiashara na jinsi ambavyo wanaweza kufaidika na mpango huo, pia ameelezea juu ya wafanyabiashara, wakulima na wajasiliamali jinsi ambavyo wanaweza kufikia malengo Makubwa, alimalizia kwa kutoa mambo makuu matatu ambayo ni pamoja na  Kuwezesha vyama vya ushirika viwe katika matukio makubwa sasa,viwe endelevu na viweze kukopesheka.
     Kutoka kushoto ni Mwalimu Shipela akiwa pamoja na wanafunzi wake wa Uyole Sekondari  wakisikiliza mafunzo kwa makini yanayohusu Benki ya NMB na Huduma zake.
     Meneja huduma kwa Wateja  Roselina Makulukulu  wa kwanza kutoka upande wa kulia akitoa elimu juu ya Akaunti mbalimbali za Kibenki zinazotolewa na Benki ya NMB .
     Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya IGurusi wakiendelea kupata elimu ya huduma za kibenki
     Mmoja ya wanafunzi akiuliza swali kwa Ofisa wa Benki ya NMB ambaye hayupo Pichani juu ya huduma za kibenki
     Wa kwanza kulia ni Ofisa wa Benki ya NMB akielezea kwa kina Juu ya Benki ya NMB
     Mmoja ya Ofisa wa Benki ya NMB Akitoa maelezo juu ya Huduma ya Akaunti ya NMB Chap Chap
    Wanafunzi kutoka  Shule ya Sekondari ya Rungwe  wakipata mafunzo ndani ya Banda la Benki ya NMB mafunzo
    Picha ya pamoja
    Na Mbeya yetu


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.