August 04, 2014

  • TANZANIA HAINA MATOKEO KABISA

    Kila siku ninapoamka, ninalazimika kuamini kuwa, kweli Tanzania haina
    matokeo, karibu kila kitu kinachofanyika Tanzania, ni sawa na hakuna
    tu, Hebu tuangalie yafuatayo, alafu tujadili na kuongeza mengine
    unayoyaona wewe;

    1. Mchakato wa katiba Mpya
    Tume iliundwa, ikaleta Rasimu ya pili ya katiba, lakini tumeingia
    kwenye BMK, tumekwama, tumekwama kwa sababu za wanasiasa kuumiliki
    mchakato, na vyama vingi kuchukulia mchakato kama mali ya chama chao.
    Mchakato una hatihati ya kufa............Tanzania hatuna matokeo

    2. Michezo
    Tumeona Taifa stars ikiangukia pua kule Msumbiji, si kule tu, michezo
    mingi hatuko kabisa kwenye ramani, Je, ni kweli hatuna wenye vipaji?
    Tatizo ni nini? Tumeenda kwenye mashindano ya jumuiya ya madola, nako
    tumesindikiza wakenya, na mataifa mengine tu...........Tanzania hatuna
    matokeo na hapo!

    3. Madini
    Mataifa yaliyona uelewa juu ya madini waliyonayo, hujiona wao ni
    wengine kutokana na ukweli kwamba hutumia bidhaa hiyo kuiendeleza
    nchi, na si kuiendeleza familia. Tanzania tunaona wawekezaji kwenye
    sekta hii ndo miungu. Wawekezaji hulipa kodi kiduchu sana, kiasi cha
    kuzidiwa na wafanyakazi wao. Napo tume-relax tu! Badala ya sisi
    kunufaika, ananufaika mwekezaji pekee huku tukidanganyana tu kwenye
    majukwaa....tukiachiwa milima na mashimo yasiyo na idadi, mito ikijaa
    sumu kutokana na maji taka ya kutoka migodini, bado tunachekelea tu,
    na tumeridhika na haya maisha..................Tanzania hatuna matokeo
    kabisa hapo!

    4. Mbuga na utalii
    Sasa watu wachache ndo wamekuwa wamiliki wa mbuga zetu, "Twiga
    anapanda Ndege, Mzaramo anapunga mkono". Hayo ndo maisha tuliyoyazoea.
    Tembo wanauwawa tu, eti kisa yale meno yake (ndovu), yaali kila upuuzi
    unaofanywa dhidi ya viumbe hawa wa Mungu. Serikali inakuja na
    kutuambia mikakati kibao, lakini mwisho wa siku, ni yale yale
    tu.....................Tanzania haina matokeo na hapo tu?

    5. Mafuta na Gesi
    Naamini nayo yatakuwa ni yale yale tu. Upuuzi ule ule tu
    utafanyika/unaendelea kufanyika................Tanzania hatuna matokeo
    bado!

    6.
    7.
    8. Mkuu wa kaya anaulizwa kwa nini Tanzania ni Masikini?, yeye anajibu
    HAJUI KWANINI Tanzania ni
    Masikini..................................Tanzania haina matokeo bado
    hata hapo jamani?
    9. malizia wewe msomaji wa hii mada..............TANZANIA HAINA
    MATOKEO KABISA.Je, unaridhika na hii hali? kuna wengi tu wanaridhika,
    hawajali ni jinsi gani Tanzania ni masikini.
    --
    Ipyana Lwinga
    Email:    ipyanalwinga@gmail.com

    "Mpende Jirani yako kama nafsi yako..."
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.