August 04, 2014

  • NHIF YAWAHIMIZA WAKAZI WA MKOA WA LINDI NA MTWARA KUPIMA AFYA ZAO




    NHIF YAWAHIMIZA WAKAZI WA MKOA WA LINDI NA MTWARA KUPIMA AFYA ZAO

    Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya Lindi vijijini,Bw Ngatiche
    akipima afya yake katika banda la NHIF alipotembelea banda hilo katika
    viwanja vya nanenane Ngongo


    Naibu waziri wa kilimo na chakula  ,Godfrey Zambi  akipokea
    maalezo mbalimbali kuhusiana na NHIF Toka kwa meneja wa mkoa wa Lindi Bi Fortunata Kullaya huku Mkurugenzi wa masoko Bw Raphae mwamoto  akisikiliza kwa umakini kuhusiana na Chf inavyofanya vizuri wilayani Nachingwea. 

     Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalotoa huduma na
    ushauri katika viwanja vya Nane nane Lindi.
     Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto akiwa

    katika Picha ya Pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Titus
    Kamani(MB) pamoja Naibu waziri wa kilimo na ushirika,Mhe Godfrey Zambi
    na Mbunge wa Jimbo la Mtwara mjini,Hasnein Murji mara baada ya
    ufunguzi wa maonesho ya nane nane mkoani Lindi.

    Na Abdulaziz-LINDI.

    Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF), umewahimiza wakazi wa
    mikoa ya Lindi na Mtwara kutembelea banda la mfuko huo kwa ajili ya
    kupima afya zao kwenye maonyesho ya wakulima 'Nanenane'.
    Wito huo umetolewa na Naibu waziri waziri wa kilimo,chakula na
    Ushirika,ZAMBI Mara baada ya kukagua banda la  la mfuko huo katika
    viwanja vya Ngongo mjini Lindi yanayofanyika kitaifa mkoani humo mwaka
    huu.

    Akiongea na waaandhishi wa habari,Naibu waziri huyo alieleza
    kuridhishwa kwake na huduma zinazotolewa na mfuko huo hususani mfuko
    wa Afya jamii(CHF) Ambao kwa aslimia kubwa umeleta tija na kupunguza
    gharama kwa wateja wake hususan Vijijini.

    'Waandishi nawaomba muendelee kuutangaza mfuko wa chf kwa kuwa umekuwa  mkombozi kwa mwananchi mwenye kipato cha chini Ni dhamira ya Serikali    kusaidia huduma hii ndio maana michango Inayochangiwa jamiii kwa kaya   Serikali nayo hutoa kiasi kama kilichongawiwa ili kuongeza ufanisi wa   dawa katika zahanati na vituo vya afya;Alimalizia Zambi.

    Akitoa taarifa ya mfuko huo,Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF,
    Raphael Mwamoto, alisema hiyo ni fursa kwa wanachama na wasio
    wanachama wa mfuko huo kujua afya zao ikiwemo kuonana na wataalamu wa    huduma za afya kwa ushauri na Tiba bila malipo na huduma zinazotolewa  ni kwa kila mmoja si kwa wanachama pekee.

    Mfuko  unaamini kuwa ni  rahisi kudhibiti magonjwa baada ya vipimo
    kuliko kusubiri kutibu ugonjwa ulioenea mwilini Na ndio maana NHIF Ipo
    kwa ajili ya jamiii tumejipanga kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo
    vipimo vya kiwango cha sukari mwilini, shinikizo la damu, saratani ya
    matiti, uzito na urefu, kisha kutoa ushauri wa kitaalam kwa
    watakaopimwa.

     'NHIF Ipo katika maonesho haya hadi siku ya mwisho unaweza fika kujua
    huduma tunazozitoa ikiwemo kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii na pia
    tuna madaktari waliobobea kuhakikisha kila anaefika katika banda letu
    anapata huduma bora"Alimalizia Mwamoto.

    Maonyesho ya Nanenane yanafanyika kitaifa mkoani Lindi katika viwanja
    vya Ngongo Maonesho yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
    baraza la Mapinduzi,Dr Ally Mohamed Shein


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.